A19, Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Njia ya A19


Barabara kuu ya A19 nchini Tanzania inaunganisha bandari za Mtwara kwenye Bahari ya Hindi na Mbamba Bay kwenye Ziwa Nyasa.

Inaanza mjini Mtwara kwenye njiapanda na barabara B2 ya kwenda Dar es Salaam[1]. Kutoka hapo inaelekea upande wa kusini magharibi kupitia Nanyamba, Tandahimba na Newala hadi Masasi. Kutoka hapao inaendelea upande wa magharibi ikipita Tunduru hadi Songea. Songea inakutana na B4 ya kwenda Njombe na Makambako.

Kuanzia Songea A19 inaelekea tena kusini-magharibi ikipita Mbinga na hatimaye kufika Mbamba Bay[2].

Urefu wote wa njia hiyo ni kilomita 816.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kigezo:Google maps
  2. Kigezo:Google maps
  3. Kigezo:Google maps