İlkay Gündoğan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
ILkay gundogan akipiga mpira.

Ilkay Gündoğan (kwa Kijerumani hutamkwa [ˈʔɪlkaɪ ˈɡʏndoːan] na kwa Kituruki [ˈilkaj ˈɟyndoːan]; amezaliwa Gelsenkirchen, tarehe 24 Oktoba 1990) ni mchezaji mahiri wa timu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ujerumani.

Alichezea academi ya VfL Bochum mwaka 2008 alianza kucheza katika klabu FC Nürnberg na baadaye akaenda kuichezea Borussia Dortmund mwaka 2011 mwaka 2013 aliisadia Borussia Dortmund kuingia katika mashindano ya klabu bingwa za Ulaya.

Alicheza mechi 157 na kufunga magoli 15 katika ligi. İlkay Gündoğan aliuzwa kwa Manchester City kwa dau la £ 21 milioni mwaka 2016 aliongoza Manchester City kuchukua kombe la ligi la mwaka 2017-2018.

Ikay Gundogan ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki kama ilivyo kwa mchezaji mwenzake Emre Can, Gundogan alizomewa na mashabiki baada ya kukutana na rais wa Uturuki na kumuita 'rais wangu'.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu İlkay Gündoğan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.