Wafiadini wa Gorkum
Mandhari
Wafiadini wa Gorkum (walifariki Brielle, Uholanzi, 9 Julai 1572, ni Wakristo 19 wanaoheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu wafiadini kwa kuwa walidhihakiwa na kuteswa kikatili wakauawa na Waprotestanti kwa kunyongwa kwa sababu walitetea imani sahihi katika ekaristi na kukataa kujitenga na Papa.
Karibu wote walikuwa mapadri, kumi na mmoja wa kwanza walikuwa Wafransisko, wengine wa mashirika mengine au wanajimbo. Mbali ya Waholanzi, wawili waliotokea Denmark na Ujerumani [1].
Majina yao ni:
- Nikola Pieck, padri wa Ndugu Wadogo
- Petro wa Assche, bruda wa Ndugu Wadogo
- Wilehadi wa Denmark, padri wa Ndugu Wadogo
- Teodoriko van der Eem, padri wa Ndugu Wadogo
- Nikasi wa Heeze, padri wa Ndugu Wadogo
- Antoni wa Hoornaert, padri wa Ndugu Wadogo
- Godefrid wa Melveren, padri wa Ndugu Wadogo
- Fransisko wa Roye, padri wa Ndugu Wadogo
- Antoni wa Weert, padri wa Ndugu Wadogo
- Jeromu wa Weert, padri wa Ndugu Wadogo
- Korneli wa Wijk-bij-Durstede, bruda wa Ndugu Wadogo
- Yohane wa Oisterwijk, padri wa Wakanoni Waaugustino
- Yohane Heer, padri wa Wadominiko
- Adriani wa Hilvarenbeek, padri wa Wakanoni Wapremontree
- Yakobo Lacops, padri wa Wakanoni Wapremontree
- Leonardi Veghel, padri mwanajimbo
- Nikola Poppel, padri mwanajimbo
- Godefrid Duynen, padri mwanajimbo
- Andrea Wouters, padri mwanajimbo
Kwanza walitangazwa na Papa Klement X kuwa wenye heri tarehe 24 Novemba 1675, halafu watakatifu na Papa Pius IX tarehe 29 Juni 1867.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai[2].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |