Ratko Janev

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ratko Janev

Ratko Janev (30 Machi 193931 Disemba 2019) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Yugoslavia.

Alisoma fizikia kwenye chuo kikuu cha Belgrad alipofikia shahada ya uzamivu mnamo 1968.

Kuanzia mwaka 1965 alifanya kazi kwenye taasisi ya utafiti wa fizikia ya nyuklia "Boris Kidrič".

Mwaka 1972 alikuwa profesa wa fizikia ya kinadharia kwenye chuo kikuu cha Belgrad.

Mwaka 1986 alihamia Vienna alipoongoza idara ya data kwenye Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia[1].

Katika miaka 2002 hadi 2004 alifanya utafiti kwenye taasisi ya fizikia ya plazma huko Jülich, Ujerumani.

Mwaka 2004 alipokea tuzo la Taasisi ya Humboldt kwa utafiti wake kuhusu "Modelling and Diagnostics of Fusion Edge / Divertor Plasmas".

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Report of the IAEA Nuclear Data Section to the International Nuclear Data Committee for the Period January – December 1999, (PDF) uk. 11

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ratko Janev kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.