Pietermaritzburg
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Pietermaritzburg | |
| Mahali pa mji wa Pietermaritzburg katika Afrika Kusini | |
| Coordinates: 29°36′36″S 30°23′24″E / Expression error: Unexpected < operator Expression error: Unexpected < operator | |
| Nchi | Afrika Kusini |
|---|---|
| Majimbo | KwaZulu-Natal |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 857,612 |
| Website: www.pietermaritzburg.co.za | |
Pietermaritzburg ni mji mkuu wa jimbo la KwaZulu-Natal katika Afrika Kusini. Ulikuwa na wakazi 230,000 mwaka 1991 waliongezeka na kukadiriwa kuwa karibu nusu milioni. Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal inafanya kazi yake Pietermaritzburg pamoja na mjini Durban. Wenyeji huuita mji mara nyingi kwa kifupi "Maritzburg" au "PMB" (tamka:pi-em-bi).
[hariri] Historia
Mji ulianzishwa na walowezi makaburu mnamo mwaka 1839. Jina lakumbusha viongozi wao Pieter Retief na Gerrit Maritz. Ilikuwa mji mkuu wa Jamhuri ya Natalia hadi kutwaliwa na Waingereza mwaka 1843 na kuwa mji mkuu wa koloni ya kiingereza ya Natal.
Baada ya uchaguzi huru wa 1994 Pietermaritzburg na Ulundi zilikuwa zote mbili miji mikuu ya KwaZulu-Natal. Baada ya ushindi wa ANC (African National Congress) jimbonio mwaka 2004 Pietermaritzburg ilikuwa mji mkuu wa pekee jimboni.