Nachingwea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mahali pa Nachingwea (kijani) katika mkoa wa Lindi.

Wilaya ya Nachingwea ni wilaya moja ya Mkoa wa Lindi. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 162,081 [1].

Wilaya hii imepakana na wilaya za Ruangwa upandw wa kaskazini Lindi Vijijini upande wa mashariki halafu na mikoa ya Mtwara na Ruvuma upande wa kusini.

Nachingwea kuna hospitali, Chuo cha Ualimu, shule za sekondari 3 na za msingi 81 wilayani.

Eneo hili lilikuwa sehemu ya mradi wa karanga wakati wa ukoloni wa Uingereza.

Kuna madini ya nikeli katika Nachingwea na kampuni ya IMX Resources NL (zamani Goldstream Mining) kutoka Australia imeanzisha kampuni "Continental Nickel" ya kuchimba nikeli hii lakini 2008 bado imetafuta pesa kwenye soko la hisa ya Kanada.


Yaliyomo

Asili ya Nachingwea [hariri]

Neno Nachingwea asili yake imetokana na mti mmoja uliokuwa ukiitwa Ngwea. Wakazi wa makao makuu ya wilaya ya Nachingwea wakati huo Ruponda walikuwa wakienda kuchota maji chingi ya mti wa Ngwea, kwa hiyo walikuwa wakisema Nachi Ngwea wakimaanisha naenda kwenye Ngwea, yaani maana yake nakwenda kuchota maji kwenye ngwea, ndipo jina hilo Nachingwea likashika kasi na kuwa Nachingwea ya leo. Makao makuu ya mwanzo ya Nachingwea yalikuwa Ruponda.

Utawala [hariri]

Wilaya ya Nachingwea ina kata zifuatazo:

Viungo vya Nje [hariri]

Picha za Nachingwea kwa Flikr [www.minebox.com/story.asp?articleId=8937 ]

Marejeo [hariri]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Nachingwea - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Nambambo | Kilimani Hewa | Ruponda | Mnero | Namapwia | Kipara Mnero | Lionja Namikango | Nditi | Kilima Rondo | Mbondo | Kiegei | Mkoka | Chiola | Mpiruka | Nangowe | Mkotokuyana | Naipanga | Stesheni | Naipingo | Mutua | Mnero Ngongo | Matekwe | Marambo | Namatula | Ndomoni