Muhammad Ali
| Muhammad Ali |
|
| Takwimu | |
|---|---|
| Jina | Muhammad Ali |
| Jina la kuzaliwa | Cassius Marcellus Clay Jr. |
| Jina la utani | The Greatest, The Champ, The Louisville Lip |
| Urefu | 1.91 m (6 ft 3 in) |
| Kufikia | 2 M |
| Mgawanyiko wa uzito | Uzito mkubwa |
| Utaifa | Marekani |
| Tarehe ya kuzaliwa | 17 Januari 1942 |
| Mahala pa kuzaliwa | Louisville, Kentucky, U.S. |
| Msimamo | Orthodox |
| Rekodi ya ndondi | |
| Jumla ya mapigano | 61 |
| Ameshinda | 56 |
| Alizoshinda kwa kuangusha | 37 |
| Alizopteza | 5 |
| Sare | 0 |
| Pambano asiloshiriki | 0 |
Muhammad Ali (amezaliwa na jina la Cassius Marcellus Clay Jr.; mnamo 17 Januari 1942) ni mwanamasumbwi mstaafu kutoka nchini Marekani. Amepata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu. Huyu anatazamika kama mmoja wa wanamasumbwi bora wa uzito wa juu wa muda wote. Wakati akiwa mwanamasumbwi wa ndondi za ridhaa, alishinda medali ya dhahabu ya uzito wa chini kwenye mashindano ya Olompiki ya mwaka wa 1960 yaliyofanyika mjini Rome, Italia. Baada ya kuwa mwanamasumbwi wa kulipwa, amekwenda kuwa mwanandondi wa kwanza kushinda mara tatu daraja la lineal. Mnamo mwaka wa 1999, Ali alipewa taji la "Mwanamichezo wa Karne" na Sports Illustrated na "Mwanamichezo Mashuhuri wa Karne" na BBC.[1]
Anafahamika sana kwa staili ya upiganaji wake, ambapo aliielezea staili yake kuwa ni "napaa kama kipepeo, nauma kama nyuki".[2]
Awali alijulikana kama Cassius Clay, lakini alibadilisha jina lake baada ya kujiunga na jumuia ya Kiislamu ya Nation of Islam mnamo mwaka wa 1964, baadaye akabadilisha dini na kuwa Mwislamu kunako mwaka wa 1975. Mnamo mwaka wa 1967, Ali alikataa kuwekwa katika orodha ya majeshi ya Marekani kutokana na imani ya kidini na kupinga vita dhidi ya Vietnam. Alikamatwa na kupatikana na hatia juu ya rasimu ya ukwepaji mashtaka, wakamvua taji lake la uwanamasumbwi, na leseni yake ya uwanamasumbwi ikazuiliwa. Hakufungwa, lakini hakupambana kwa takriban miaka minne mpaka hapo rufaa yake ilipofanyiwa kazi na Mahakama Kuu ya Marekani, ambapo akaja kushinda.
Tanbihi [hariri]
Marejeo [hariri]
- Hauser, Thomas (2004). Muhammad Ali: His Life and Times. Robson Books. ISBN 1861057385. OCLC 56645513.
Viungo vya Nje [hariri]
- www.ali.com Official website
- Top Ali Fight Photos from Sports Illustrated
- Muhammad Ali at the Internet Movie Database
- www.maprc.com Muhammad Ali Parkinson Center (MAPC)
- Muhammad Ali: Made in Miami
| Makala hii kuhusu mtu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muhammad Ali kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |