Msitu wa Magoroto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Magoroto ni msitu maarufu wa Kitropiki unaopatikana katika wilaya ya Muheza, mkoa wa Tanga. Awali msitu wa Magoroto ulikuwa mashamba ya watawala wa Kijerumani na baadaye ukahifadhiwa kama sehemu muhimu yenye uoto wa asili. Upekee wake ni kuwepo kwa ziwa lililotengenezwa na binadamu lenye viumbehai mbalimbali, wakiwemo samaki.[1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Msitu huo, wenye ukubwa wa ekari 591 na ziwa la maji safi, ulifunguliwa mwaka 1896 na watalawa wa Kijerumani kama shamba la kwanza la kibiashara Afrika Mashariki. Kwa mara ya kwanza shamba hilo lililima zao la mpira baada ya kushindwa kulima kahawa na chai na baadaye kulimwa michikichi mwaka 1921.

Eneo hilo lilichukuliwa na wazawa “kundi la Amboni” mwaka 1940 na kilimo cha michikichi kilisitishwa baada ya kuwepo ushindani kati ya Malaysia na Indonesia. Baada ya hapo, Msitu wa Magoroto ulihifadhiwa mpaka leo kwa kuzingatia upekee na uzuri wake.

Pamoja na kupakana na msitu wa Mlinga, Magoroto inatengeneza vipande vya milima ya Usambara ambayo inafahamika kwa uzuri na upekee wa uoto wa asili. Unafahamika zaidi kwa uwepo wa ndege wa pekee ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Chama cha Uhifadhi Wanyamapori wanahusika katika uhifadhi wa misitu hiyo nchini.[2]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Msitu wa Magoroto kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.