Mnara wa Eiffel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mnara Eiffel
Mnara wa Eiffel

Mnara wa Eiffel (kwa Kifaransa: Tour Eiffel) ni jengo mashuhuri la mji wa Paris nchini Ufaransa.

Mnara huu ulipokea jina lake kutoka kwa mjenzi wake aliyekuwa mhandisi Alexandre Gustave Eiffel.

Kimo chake ni mita 300 na juu yake kuna antena ya redio jumla ya kimo inafikia mita 324.

Mnara huu ulijengwa kando ya mto Seine miaka 1887 hadi 1889 kama geti la Maonyesho ya Dunia ya mwaka 1889.

Mwanzoni watu wa Paris hawakupenda mnara huo: wengine walidai ubomolewe mara moja baada ya maonyesho. Lakini idadi kubwa ya watalii iliufanya kuwa ishara ya mji wa Paris na watu walianza kuuzoea.

Kati ya miaka 1889–1930 ilikuwa jengo kubwa la dunia nzima.

Mwaka 1906 mnara uliwezesha mawasiliano ya kwanza kwa simu hewa kati ya Ulaya na Marekani kuvukia Atlantiki kwa sababu ya kimo chake kikubwa. Wanajeshi walikuwa na kituo cha mawasiliano ya simu mnarani.

Kila mwaka hutembelewa na wageni milioni sita wanaoipanda kwa kutumia ngazi 1,665.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Ufaransa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mnara wa Eiffel kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.