Mikoa ya Kamerun

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mikoa ya Kamerun

Mikoa ya Kamerun ni maeneo ya utawala wa ngazi ya juu nchini Kamerun. Kwa lugha ya Kifaransa huitwa "région" tangu mwaka 2008 ambapo rais Paul Biya alibadilisha jina rasmi kutoka "provinces" za awali kuwa "régions. Jumla ya mikoa ni 10.

Mikoa hiyo hugawiwa katika wilaya (kwa Kifar. départements) 58. Ndani ya wilaya kuna tarafa (arrondissements) 360, manispaa (municipalités) na maeneo ya kichifu (chefferies).

Kila mkoa uko chini ya mkuu wake anayeitwa gavana (gouverneur de région) na kuteuliwa na rais wa jamhuri, pamoja na Halmashauri ya Mkoa.

Halmashauri ya Mkoa ni serikali ya mkoa. Ina wawakilishi wa wilaya wanaochaguliwa na wawakilishi wa watawala wa jadi.