Nenda kwa yaliyomo

Marina Alois Njelekela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Marina Alois Njelekela (alizaliwa 23 Julai 1964) ni mwanamke anayefahamika kwa kampeni mbalimbali za kupambana na saratani ya kizazi na matiti nchini Tanzania, zilizofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Lindi, Dodoma na Manyara.[1]

Ni mtoto wa kike katika familia ya Alois Simon na Bernada Sunzi (Kapinga) Njelekela.

Elimu yake

[hariri | hariri chanzo]

Alihitimu mafunzo ya udaktari wa dawa katika chuo kikuu cha Muhimbili, Dar es Salaam mwaka 1993 na kupata shahada ya uzamivu katika chuo kikuu cha Kyoto, Japani mwaka 2003.[2]

Kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Alifanya mafunzo, Tanzania Consultant Teaching Hospital, iliyopo Kilimanjaro mwaka 1993-1994. Mwaka 1994-1995 akawa msajili katika hospitali ya Agakhan iliyopo Dar es salaam, halafu daktari wa dawa katika hospitali ya wilaya ya kisarawe, mkoa wa Pwani mwaka 1995-1996.

Mwaka 1996-2001 alikuwa msajili katika taasisi ya mifupa ya Muhimbili, Dar es Salaam, halafu msaidizi wa mafunzo ya fiziolojia katika chuo kikuu cha Muhimbili mwaka 2001-2002 na hatimaye kuwa mhadhiri wa fiziolojia tangu mwaka 2003.[3]

Uanachama

[hariri | hariri chanzo]

Marina Njelekela alikuwa mwenyekiti wa Medical Women Association Tanzania kwa kipindi cha miaka sita na pia mwanachama wa Japan society nutrition and food science.

Tuzo zake

[hariri | hariri chanzo]

Alipata tuzo mbalimbali kutokana na juhudi zake za kuboresha afya kwa akina mama na watoto Tanzania ikiwemo Tuzo ya Martin Luther King.[4]