Kiongozi Kalenda
Kiongozi Kalenda ni kijitabu chenye chaguo cha maneno kutoka Biblia kwa kujisomea kila siku. Maneno haya hutazamiwa kama "maneno ya mwongozo wa kiroho" kwa ajili ya siku husika. Hutolewa na Kanisa la Moravian katika nchi nyingi duniani kwa lugha zisizopungua 50. Jina lake la Kiingereza ni "Daily Watchwords" na kwa Kijerumani "Losungen". Hutolewa upya kila mwaka.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kalenda hii ilianzishwa tar. 3 Mei 1728 huko Herrnhut, Ujerumani na hadi leo ni mwongozo wa kiroho inayosomwa na watu wengi kila siku. Ingawa tangu mwanzo ilitolewa na Kanisa la Moravian leo hii hutumiwa katika nchi mbalimbali pia na Wakristo wasio Wamoravian. Kwa jumla makala milioni 1.5 huchapishwa na kuuzwa kila mwaka ambayo ni zaidi kuliko jumla la Wamoravian duniani.
Aliyeanzisha kalenda ni Nikolaus Ludwig von Zinzendorf aliyewapa ndugu wa ushirika wa kwanza wa Moravian neno la Biblia kama mwongozo kwa siku ya 3 Mei. Tangu siku ile ndugu moja alizunguka kila asubuhi katika nyumba zote 32 za kijiji cha Herrnhut akiwaambia wenzake neno lililowahi kuteuliwa kwa siku ile. Mwaka 1732 maneno ya Biblia yalitolewa mara ya kwanza kwa siku zote za mwaka na kuchapishwa kama orodha katika kitabu.
Mwanzoni von Zinzendorf mwenyewe alichagua maneno kwa ajili ya kila siku. Kwa kila siku ya mwaka aliteua aya ya Biblia pamoja na beti ya nyimbo ya kiroho. Baadaye uteuzi huu ulufanywa katika mkutano wa ushirika wa Herrnhut.
Kuteuliwa kwa maneno ya mwongozo
[hariri | hariri chanzo]Siku hizi kuna kamati ya watu 6 inayokutana huko Herrnhut kila mwaka karibu na tarehe ya 3 Mei ambayo ni tarehe ya kihistoria ambako neno la mwongozo la kwanza lilitolewa. Kati ya hao watu 6 kuna watumishi wa kamati kuu ya Wamoravian wa Ulaya Bara pamoja na wakristo wengine. Wanafungua mkusanyo wa ayat 1.829 kutoka Agano la kale zilizoteuliwa kwa ajili ya kalenda na kuandikwa juu ya vikaratasi. Kwa kila siku wanatoa karatasi 1 bila kuisoma kwanza. Baadaye kamati inatafuta neno kutoka Agano Jipya linalolingana na maana ya neno la kwanza na pia beti ya wimbo la kiroho linalofaa au maneno ya sala.
Kazi hii hufanywa miaka miwili na nusu kabla ya mwaka husika kwa sababu muda inahitajika kuandika chaguo, kuituma katika nchi zote ambako maneno ya mwongozo hutolewa kwa lugha nyingine hadi kuchapishwa. Kwa mfano maneno ya mwaka 2012 yalitolewa tar. 23 Aprili 2009 huko Herrnhut.
Katika Tanzania kuna kamati ya KMT inayotumia orodha ya kiingereza na kuchagua ayat ya Biblia ya Kiswahili ipasavyo. toleo la kiswahili hadi sasa haina maneno ya sala au mabeti ya nyimbo. Kuna sehemu nyingine za Biblia zinazopendekezwa kwa wasomaji wanaopenda kujisomea Biblia kufuatana na utaratibu fulani.
Maneno ya Kiongozi Kalenda kwa lugha mbalimbali
[hariri | hariri chanzo]Lugha | Jina la Kiongozi Kalenda kwa lugha hii | Imetolewa tangu |
Kiafrikaans | Teksboek van die Broederkerk | |
Kialbania | 2005 | |
Kiingereza cha Marekani | Daily Texts of the Moravian Church – Daily Watchwords | 1743 |
Kiamhari | ||
Kiarabu | ||
Kibali (Indonesia) | ||
Kibassa (Kamerun) | ||
Kibatak (Indonesia) | ||
Kibulgaria | ||
Chichewa (Malawi) | ||
Kichina | Christian Watch-Word | |
Kidenmark | Løsensbogen | |
Kijerumani | Die täglichen Losungen und Lehrtexte der Brüdergemeine | 1731 |
Kiingereza | Daily Watchwords -(The Moravian Text Book) | 1740 |
Kiestonia | Vaimulikud loosungid | |
Kifini | Päivän Tunnussana | 1905 |
Kifaransa | Paroles et Textes | 1741 |
Kigiriki (Agano Jipya pekee) | Ursprachenausgabe Losungen (Toleo kwa lugha asilia ya Biblia) | 1995 |
Kiebrania (Agano la Kale pekee) | Ursprachenausgabe Losungen (Toleo kwa lugha asilia ya Biblia) | 1995 |
Kindonesia | ||
Kiinuktitut (Kieskimo - Greenland) | ||
Kiisilandi | 2006 | |
kiitalia | Letture Quotidiane Bibliche dei fratelli moravi; Un giorno, una parola | |
Kijapan | ||
Kikorea | 2009 | |
Kikroatia | ||
Kilatvia | Lozungi | |
Kilithuania | ||
Kimayangna (Maindio wa El Salvador, Nicaragua na Honduras) | 2007 | |
Kimiskito (Maindio wa Nicaragua na Honduras) | Yua Bani Bila Nani | |
Kinepali | ||
Kiholanzi | Dagteksten | |
Kioriya (Orissa, Uhindi) | ||
Oshivambo (Namibia) | ||
Sepedi (Afrika Kusini) | ||
Kipoland | ||
Kireno | Meditações Diàrias | |
Rongmei (Assam, Uhindi) | ||
Kinyarwanda (Ruanda) | ||
Kiromania | ||
Kirusi | Slowa Schtschisni | |
Kisweden | Dagens Lösen | |
Setswana (Botswana) | ||
Siswati (Afrika Kusini) | ||
Kislovakia | ||
Kisorbi (Ujerumani) | ||
Kihispania | Devocionales Diarios | |
Kiswahili | Kiongozi Kalenda | |
Kisurinam | Bijbel-Almanak ofoe Dei Boekoe | |
Kitibet | ||
Kicheki | Hesla Jednoty Bratrské | |
Kituruki | ||
Kihungaria | Utmutató | |
Tshivenda (Afrika Kusini) | ||
isiXhosa (Afrika Kusini) | Isalatiso Se-Moriva | |
isiZulu (Afrika Kusini) |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Kiongozi kalenda katika intaneti kwa lugha ya Kiswahili Ilihifadhiwa 1 Januari 2011 kwenye Wayback Machine.
- Huduma ya Kanisa la Moravian Marekani inayotuma neo la mwongozo kila siku kwa barua pepe