Jumamosi kuu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu maarufu ya Pietà ya Michelangelo iliyochongwa katika marumaru kuonyesha Bikira Maria akipakata maiti ya mwanae Yesu mara baada ya kifo chake.
Jumamosi kuu ni siku ya Juma kuu inayoadhimisha hasa pumziko la mwili wa Yesu Kristo kaburini kabla ya kufufuka mtukufu usiku wa Pasaka.
Tarehe yake inabadilikabadilika kila mwaka na hata mwaka uleule ni tofauti katika madhehebu ya Ukristo, hasa yanayofuata mapokeo ya mashariki na yale yanayofuata mapokeo ya magharibi.
Siku hiyo wafuasi wa Yesu wanatulia kimya wakitafakari matukio ya Ijumaa kuu na kujiandaa washangilie ufufuko wake kuanzia kesha la Pasaka hadi Jumapili ya Pentekoste siku 50 baadaye.
Majina katika lugha mbalimbali [hariri]
Jumamosi kuu inaitwa kwa namna tofauti katika lugha mbalimbali. Baadhi ya mifano ni kama ifuatavyo:
| Lugha | Jina | Tafsiri |
|---|---|---|
| Kicheki | Bílá sobota | Jumamosi nyeupe |
| Kifaransa | Samedi saint | Jumamosi takatifu |
| Kihispania | Sábado Santo | Jumamosi takatifu |
| Kiholanzi | Stille Zaterdag | Jumamosi ya kimya |
| Kihungaria | Nagyszombat | Jumamosi kuu |
| Kiingereza | Holy Saturday | Jumamosi takatifu |
| Kiitalia | Sabato Santo | Jumamosi takatifu |
| Kijapani | 聖土曜日 (Sei Doyoobi) | Jumamosi takatifu |
| Kijerumani | Karsamstag | Jumamosi ya ombolezo |
| Kipolandi | Wielka Sobota | Jumamosi kuu |
| Kislovakia | Biela sobota | Jumamosi nyeupe |