Juliani wa Le Mans

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dirisha la vioo vya rangi likimuonyesha Mt. Julian wa Le Mans na matukio 16 ya maisha yake (karne ya 12, lilikarabatiwa mwaka 1897) - Kanisa kuu la Le Mans (Sarthe, Ufaransa).

Juliani wa Le Mans alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo (leo nchini Ufaransa).

Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 27 Januari[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alipewa uaskofu huko Roma, Italia, katikati ya karne ya 3 akatumwa Galia kuinjilisha kabila la Wasenomani. Alipofika kwao alijivutia mioyo yao kwa huduma zake kwa maskini, wagonjwa na mayatima, mbali ya miujiza mbalimbali.

Alipofikia uzee alikwenda kuishi kama mkaapweke.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.