Holili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Holili ni kata ya Wilaya ya Rombo katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10,932 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,299 [2] walioishi humo.

Holili kwa upande wa mashariki inapakana na Taveta (Kenya), upande wa kaskazini inapakana na kata ya Mahida, kusini inapakana na wilaya ya Mwanga na upande wa magharibi inapakana na wilaya ya Moshi vijijini.

Wakazi asili wa Holili ni Warombo na jina Holili linasemekana kutokana na neno la Kiseri "Ulili" ikiwa na maana ya "Kitanda" kwa Kiswahili.

Kilometa tatu kaskazini magharibi mwa mji mdogo wa Holili upo mlima unaoitwa "Manuo" ikiwa ni neno la Kiseri lenye maana ya "mawe ya kunolea" na pia unaitwa "maimbu" ikiwa ni jina la mtu aliyeishi hapo miaka ya zamani.

Holili ndiyo inayoongoza Tanzania kwa kuwa na rasilmali ya madini aina ya pozolana yanayotumika kutengenezea saruji.

Biashara kubwa humo ni ubadilishanaji wa bidhaa na nchi jirani ya Kenya, mchanga na matofali.

Pia ziko biashara ndogondogo za mama ntilie, vilabu vya pombe na vyumba vya kulala wageni, kilimo na ufugaji mdogomdogo.

Kuna ofisi na vituo vya pamoja vya forodha vya jumuia ya Afrika Mashariki.

Holili pia kuna shule tatu za msingi ambazo ni: shule ya msingi Holili, shule ya msingi Kastamu na shule ya msingi Ritaliza.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Rombo DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-23. 
Kata za Wilaya ya Rombo - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania

Aleni | Chala | Holili | Katangara/Mrere | Kelamfua/Mokala | Kingachi | Kirongo Samanga | Kirwa Keni | Kisale Msaranga | Kitirima | Mahida | Makiidi | Mamsera | Manda | Marangu Kitowo | Mengeni | Mengwe | Motamburu Kitendeni | Mrao Keryo | Nanjara | Ngoyoni | Olele | Reha | Shimbi | Shimbi Kwandele | Tarakea Motamburu | Ubetu Kahe | Ushiri Ikuini

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Holili kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.