Dola la Roma Magharibi
Kutoka Wikipedia
Dola la Roma Magharibi ni sehemu ya Dola la Roma upande wa Magharibi iliyo na mji mkuu wa Roma. Kuanzia mwaka wa 285 kulikuwa na Makaisari wawili ili kurahisisha utawala wa dola iliyokuwa kubwa mno. Chini ya Konstantin Mkuu, mji wa Konstantinopoli pia ukawa mji mkuu. Baada ya kifo cha Theodosius Mkuu, kweli kulikuwa na madola mawili yenye miji mikuu miwili. Romulus Augustus alipoondoshwa madarakani mwaka wa 476, Dola la Roma Magharibi lilikwisha.

