24 (msimu wa 5)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msimu wa 5 wa 24

Season 5 Cast
Nchi asilia Marekani
Mtandao Fox Broadcasting Company
Iko hewani tangu 15 Januari 2006 – 22 Mei 2006
Idadi ya sehemu 24
Tarehe ya kutolewa DVD 5 Desemba 2006
Msimu uliopita Msimu wa 4
Msimu ujao Msimu wa 6

Msimu wa Tano (pia unajulikana kama Siku ya 5) ya mfululizo wa kipindi cha televisheni cha 24 kilichoanza kurushwa hewani kuanzia tar. 15 Januari 2006 na kumalizia msimu wake kunako tar. 22 Mei 2006.

Hadithi ya Msimu wa Tano inaanza na kushia 7:00 asubuhi. Muda wake uko sawa na ule wa msimu uliopita.

Dakika 10 za mwanzo zilikuwa zikipatikana kwenye DVD ya msimu uliopita.[1] Ilikuwa ikirushwa kwenye Sky One huko nchini Uingereza kabla ya kuanza rasmi kwa msimu wa tano.

Muhtasari wa Msimu[hariri | hariri chanzo]

Msimu wa Tano (2006) ni seti ya miezi 18 baada ya Msimu wa Nne.

Baada ya matukio ya Msimu wa Nne, kachero wa CTU Jack Bauer sasa hivi anafanyakazi siku-hadi-siku akiwa kama mfanyakazi wa kampuni ya kusafisha mafuta akiwa chini ya jina la "Frank Flynn" mjini Mojave, California. Jack arejea zake nyumbani huko mjini kaskazini mwa mji wa Los Angeles kwa Diane Huxley, mama asiye na mume, na mtoto wake mwenye umri miaka 15 aliyeitwa Derek.

Msimu wa Tano ilitakiwa iwe siku kubwa katika kipindi cha urais cha Charles Logan. Amepanga kusaini mkataba wa muungano kupinga ugaidi na Rais wa Urusi Bw. Yuri Suvarov kwa hiari yake huko mjini Hidden Valley, California. Hii ni siku ambayo inaaminika kwamba iliendeshwa kinyume sana kuliko matukio ya siku zote, kama Mrusi gaidi aliyejitenga na serikali yake (imekihiswa kuwa Chechen, ingawa hili halijaelezwa vizuri) ambaye yeye ndiye aliyebeba mzigo mzima wa mashambulizi kwa imani ya kuwa mkataba ule utaumiza watu zao.

Baadaye, ikagundulika kwamba yale matukio yaliyotokea ni sehemu kubwa sana ya njama za kiserikali ya rais alioko madarakani Bw. Rais Charles Logan, Mkubwa wa Wafanyakazi Walt Cummings, mkandarasi wa Kitengo cha Ulinzi Christopher Henderson, kwa ushirikiano wa James Nathanson, na kundi la watu ambao hawajulikani wanaongoza na kushawishi matendo ya Logan watokao katika sehemu zisizojulikana, wakiongozwa na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la "Graham" ambaye inawezekana ndiye aliyefanya mpango wa Jack kujifichua kutoka mafichoni, na matukio yote.

Mpango wao wa awali ulikuwa kuachia gesi ya neva juu ya magaidi wa Kirusi na kutumia msamaha huo kama maombi ya kuachia vikosi vya kijeshi vya kupinga mkataba wa ugaidi, na kumruhusu Logan kulinda maslahi ya petroli ya Kimarekani huko Asia ya Kati. Rais wa zamani David Palmer alianza kulijua hili na akauawa ili kumnyamazisha; kifo chake kimekuwa mhamasiko mkubwa kwa harakati za Jack (mbali ya kusingiziwa kumwua David Palmer). Kama jinsi alivyoeleza kwa mara kadhaa kwenye mzunguko wa siku, "Haya mambo binafsi."

Njama kuu[hariri | hariri chanzo]

Njama ndogo[hariri | hariri chanzo]

Wahusik wa Msimu[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya washiriki wakuu wa Msimu wa 5. Tazama Orodha ya wahusika wa 24 kwa orodha iliyokamili.

Manyota

Special Guest Stars

Wageni Maalumu Waliouza Sura

Wanaojirudia

Vifo[hariri | hariri chanzo]

Msimu huu ni maarufu sana kwa idadi kubwa wahusika wakuu wanaouawa. Vifo vikubwa kabisa ni pamoja na cha David Palmer, Michelle Dessler, na Edgar Stiles. Tony Almeida aliuawa vilevile, ingawa kifo chake kilikuja kujulikana zaidi kwenye msimu wa saba. Wahusika wengine wadogo waliokufa ni pamoja na Walt Cummings na Lynn McGill. Aaron Pierce pia ilikuwa auawe, lakini Martha Logan aliona nini kilikuwa kinataka kutokea na kusaidia kuzuia lisitokee; kwa maana hiyo, Pierce ni muhusika pekee mwingine mbali na Jack Bauer kuonekana kwenye misimu yote saba ya mfululizo huu wa 24.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]