Zoe Saldana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zoe Saldana

Saldana, mnamo Julai 2014
Amezaliwa 19 Juni 1978 (1978-06-19) (umri 45)
New Jersey, Marekani[1][2]
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 1999–mpaka sasa
Tovuti rasmi

Zoé Yadira Zaldaña Nazario[1][3] (anafahamika zaidi kama Zoe Saldana, wakati mwingine huandikwa Zoë[4]; amezaliwa 19 Juni 1978) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Alipata uhusika wake katika filamu ya mwaka wa 2000 Center Stage, na baadaye kupata umaarufu zaidi kwa uhusika wa Anamaria kwenye Pirates of the Caribbean: Curse of the Black Pearl, Uhura kwenye filamu ya mwaka wa 2009 Star Trek, na Neytiri kwenye filamu ya James Cameron Avatar. Mwaka wa 2010, ameonekana kwenye filamu ya The Losers na Takers.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Saldana alizaliwa kama Zoé Yadira Zaldaña Nazario huko mjini Passaic, New Jersey,[2][5] Marekani, na Aridio Zaldaña, Mdominika, na Asalia Nazario, M-Puerto Rika.[6][7][8][9]

Lugha yake ya kwanza ni Kiingereza na Kihispania. Ametumia utotoni mwake akikulia huko mjini Queens, New York. Akiwa na umri 10, alihamia Jamhuri ya Dominika, ambapo waliishi kwa miaka mingine saba. Saldana amejiunga katika darasa la ballet katika moja kati ya shule za dansi za majigambo katika Jamhuri ya Dominika. Baada ya kurudi mjini Queens akiwa na umri wa 17, akaanza kutumbuiza kikindi cha kibisa cha Faces, ambacho kinachohusisha na michezo ya kusambaza ujumbe wa kheri kwa vijana, kupitia mandhari yanayohusiana na masuala ya utumiaji wa dawa za kulevya na ngono kwa ujumla. Michezo hiyo haikumpa uzoefu wa haja tu bali ilikuwa chanzo cha majivuno na sifa kubwa kwake, pindi alipogundua ya kwamba analeta mabadiliko katika maisha ya vijana wa lika lake. Wakati anatumbuiza na kikundi cha kibisa cha Faces na pia New York Youth Theater Zoe akachaguliwa na wakala wa vipaji. Mafunzo yake ya dansi katika miaka ya awali, jumosha na uzoefu wake wa uigizaji, kumemsaidia vilivyo kuwekza kucheza vyema uhusika wake wa kwenye skrini kubwa akiwa kama Eva, akiwa kama mcheza ballet mwenye kipaji na ushapavu katika filamu ya mwaka wa 2000 Center Stage.

Tar. 30 Juni 2010, imetangazwa kwenye Us Weekly kwamba Saldana amevishwa pete na bwana wake wa miaka 10, mwigizaji na CEO wa My Fashion Database Keith Britton.[10]

Filmografia[hariri | hariri chanzo]

Filamu
Mwaka Filamu Uhusika Maelezo
2000 Center Stage Eva Rodriguez Kama Zoë Saldana
2001 Get Over It Maggie Kama Zoë Saldana
Snipes Cheryl aka Prolifik
2002 Crossroads Kit Kama Zoë Saldana
Drumline Laila Kama Zoë Saldana
2003 Pirates of the Caribbean: The Curse of the Black Pearl Anamaria
2004 The Terminal Dolores Torres Kama Zoë Saldana
Haven Andrea
Temptation Annie
2005 Constellation Rosa Boxer
Guess Who Theresa Jones Kama Zoë Saldaña

Amechaguliwa kwa ajili ya Black Movie Award

Amechaguliwa kwa ajili ya Black Reel Award

Amechaguliwa kwa ajili ya Image Award

Dirty Deeds Rachel Buff Kama Zoe Saldaña
La maldición del padre Cardona Flor Kama Zoe Saldaña
2006 Premium Charli
Ways of the Flesh Donna aka The Heart Specialist
2007 After Sex Kat
Blackout Claudine
2008 Vantage Point Angie Jones Kama Zoë Saldana
2009 Star Trek Nyota Uhura Kama Zoë Saldana

Amechaguliwa kwa ajili ya ALMA Award

Amechaguliwa kwa ajili ya Teen Choice Award

The Skeptic Cassie
Avatar Neytiri Empire Award for Best Actress

Saturn Award for Best Actress

Amechaguliwa kwa ajili ya National Movie Award

Amechaguliwa for a Black Reel Award

Amechaguliwa for an Image Award

2010 The Losers Aisha As Zoë Saldana
Takers Rachel Jansen
Death at a Funeral Elaine Amechaguliwa- Teen choice award: Actress Comedy
Burning Palms Sara Cotton Inahaririwa
2011 Colombiana[11] Cat ipo matengenezoni
2012 Untitled Star Trek Sequel Nyota Uhura Kama Zoë Saldana
TBA Avatar 2 Neytiri Being Written
Televisheni
Mwaka Jina Uhusika Maelezo
1999 Law & Order Uncredited Sehemu: Refuge, Part 1
2004 Law & Order: Special Victims Unit Gabrielle Vega Sehemu: "Criminal"
2006–2007 Six Degrees Regina Sehemu 5

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Zoe Saldana Biography (1978-). Iliwekwa mnamo 2008-10-16.
  2. 2.0 2.1 The Official Website of Zoe Saldana — Biography. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-03-23. Iliwekwa mnamo 2010-10-10.
  3. "Zoe Saldana, con la crítica a sus pies", 2010-01-04. Retrieved on 2010-01-16. (Spanish) Archived from the original on 2010-01-18. 
  4. For the spelling and her own pronunciation of her professional name, please see: YouTube — Conversation with Avatar's James Cameron and stars Sam Worthington and Zoe Saldana.. Iliwekwa mnamo 2010-01-07. It is linked from the official website of Avatar.
  5. Jason Buchanan (2008). Zoe Saldana:Biography on MSN. MSN. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-01-29. Iliwekwa mnamo 2008-07-29.
  6. PopEntertainment.com: Zoe Saldana interview about 'Haven.' (2006-09-12). Iliwekwa mnamo 2010-01-04. “My mom is Puerto Rican and my father is Dominican.”
  7. Balfour, Brad. "HAVEN : An Interview with Zoe Saldana", Blackfilm, Septemba 2006. Retrieved on 2010-01-04. "ZS: My mom is Puerto Rican and my father is Dominican." 
  8. Boucher, Geoff (2009-11-23). 'Avatar' star Zoe Saldana says the movie will match the hype: 'This is big'. Iliwekwa mnamo 2010-01-04. “My family background is from the Dominican Republic and Puerto Rico”
  9. "ZOE SALDANA TRABAJO DE ESTRELLA", El Nuevo Herald, 2003-10-02. Retrieved on 2010-04-19. 
  10. "Avatar's Zoe Saldana Is Engaged!", UsMagazine.com. 
  11. http://www.imdb.com/title/tt1657507/

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: