Nenda kwa yaliyomo

Ziwa Great Bear

Majiranukta: 66°N 121°W / 66°N 121°W / 66; -121
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa Great Bear
Great Bear Lake
Picha ya Ziwa Great Bear kutoka angani (angalia moshi wa moto wa misituni)
Picha ya Ziwa Great Bear kutoka angani (angalia moshi wa moto wa misituni)
Mahali 66°N 121°W / 66°N 121°W / 66; -121
Nchi zinazopakana Kanada, Northwest Territories
Eneo la maji km2 31,153
Kina cha chini m 71

Ziwa Great Bear (kwa Kifaransa: Grand lac de l'Ours; "Ziwa kubwa la dubu") ni ziwa lililopo katika misitu ya Kanada ya Kaskazini.

Ni ziwa kubwa kabisa ndani ya Kanada, isipokuwa (Ziwa Superior na Ziwa Huron ambayo yanavuka mpaka wa Kanada na Marekani ni makubwa zaidi), ni ya nne kwa ukubwa Amerika Kaskazini, ni ya nane kwa ukubwa ulimwenguni.

Ziwa liko katika maeneo ya Northwest Territories, ndani ya mzingo aktiki kati ya nyuzi 65 hadi 67 za latitudo ya kaskazini na kati ya nyuzi 118 na 123 za longitudo ya magharibi ilhali liko mnamo mita 156 juu ya usawa wa bahari.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]
Ramani inaonyesha kina cha Ziwa la Great Bear.
Beseni la Mto Mackenzie likionyesha mahali pa Ziwa Great Bear katika Aktiki ya Kanada.

Ziwa lina eneo la maji la kilomita za mraba 31,153. Kina kirefu zaidi ni m 446 na kina cha wastani m 71. Beseni lake ni la km² 114,717. [1]

Ziwa Great Bear limefunikwa na barafu kutoka mwishoni mwa Novemba hadi Julai.

Mito inayoingia mle

[hariri | hariri chanzo]

Mito inapita kwenye Ziwa Great Bear ni pamoja na Mto Whitefish, Mto Big Spruce, Mto Haldane, Mto Bloody River, Mto Sloan, Mto wa Dease na Mto Johnny Hoe.

  1. "Great Bear Lake". World Lakes Database. International Lake Environment Committee. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Juni 2011. Iliwekwa mnamo 2 Februari 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Kanada bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Great Bear kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.