Nenda kwa yaliyomo

Zenoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Zenoni
Jina la Elementi Zenoni
Alama Xe
Namba atomia 54
Mfululizo safu Gesi adimu
Uzani atomia 131.293
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 161.4 K (-111.7 °C)
Kiwango cha kuchemka 165.03 K (-108.12 °C)
Asilimia za ganda la dunia 2 · 10-9 %
Hali maada gesi

Zenoni ( kut. kigiriki ξένος ksenos “kigeni” kwa sababu wafumbuzi wa kwanza waliikuta mahali wasipoitegemea) ni elementi yenye namba atomia 54 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 131.293. Alama yake ni Xe.

Ni gesi adimu inayopatikana katika angahewa haina rangi wala herufu. Kama gesi adimu zote ni bwete na kutomenyuka kirahisi na kitu kingine;

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Matumizi yake ni hasa katika aina mbalimbali za taa kwa sababu inasaidia balbu kuwa na mwanga mkali zaidi. Magari ya kisasa mara nyingi hutumia balbu za Zenoni zinatotoa mwanga mkali kwa matumizi madogo ya umeme.

Zenoni hutumiwa pia kwa vyombo vya angani kama kisukumaji. Kama gesi bwete haimenyuki na tangi na mapipa; kwa kanieneo kubwa hukaa thabiti kama kiowevu hadi halijoto ya chumbani; inageuzwa rahisi kuwa tena gesi kwa ajili ya injini.