Yohane Righi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yohane Batista Righi wa Fabriano (Fabriano (Ancona), 1469 circa – Cupramontana (Ancona), 1539) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki kutoka Italia.

Anaheshimiwa kama mwenye heri hasa tarehe 11 Machi.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kisha kuzaliwa Fabriano katika familia ya kisharifu, Yohane alifuata Ukristo tangu utotoni.

Kisha kuahidi kufuata kanuni iliyoandikwa na Fransisko wa Asizi, aliishi katika konventi ya Forano.

Halafu akawa mkaapweke katika pango «La Romita», karibu na Massaccio.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]