Yo-Yo Ma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yo-Yo Ma akipiga selo huko Davos mnamo mwaka 2008

Yo-Yo Ma ( amezaliwa 7 Oktoba 1955) ni mpiga selo kutoka nchini Marekani . Alizaliwa nchini Ufaransa na wazazi Wachina. Yo-Yo Ma ni mmoja wa wasanii wa selo wakubwa zaidi duniani. Anapiga muziki wa aina nyingi na alifabnya muzki wake mbele ya marais watatu wa Marekani .

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Yo-Yo Ma alizaliwa huko Paris . Wazazi wake walikuwa Wachina. Mama yake, Marina Lu, alikuwa mwimbaji, na baba yake, Hiao-Tsiun Ma, alikuwa profesa wa muziki. Familia yake ilihamia New York alipokuwa na umri wa miaka minne.

Ma alianza kusoma fidla alipokuwa mdogo sana. Pia alipiga viola kwa muda mfupi. Alipokuwa na umri wa miaka minne alianza kujifunza selo . Alianza kutumbuiza mbele ya wasikilizaji akiwa na umri wa miaka mitano. Alipokuwa na umri wa miaka saba alimtumbuiza Rais John F. Kennedy . Akiwa na umri wa miaka minane alishiriki katika tamasha lililoongozwa na Leonard Bernstein . Kufikia umri wa miaka kumi na tano, Ma alikuwa amehitimu kutoka Shule ya Utatu huko New York na alionekana kama mpiga selo wa pekee katika Orchestra ya Harvard Radcliffe akipiga "Variations on a Rococo Theme" ya Tchaikovsky .

Ma alisoma katika Shule ya Muziki ya Juilliard . Mwalimu wake alikuwa Leonard Rose . Alienda Chuo Kikuu cha Columbia na kisha Chuo Kikuu cha Harvard .

Ma alioa mnamo 1977. Wanandoa hao wana watoto wawili. Wanaishi Cambridge, Massachusetts .

Ma anatumbuiza katika Ikulu ya Marekani (kushoto kwenda kulia, walioketi) Rais Ronald Reagan, Binti wa Kifalme Michiko na Mwanamfalme Akihito wa Japani, na Mke wa Rais Nancy Reagan, 1987

Ma anavutiwa na muziki kutoka tamaduni tofauti. Ana kikundi kiitwacho Silk Road Ensemble ambacho kinajaribu kuunganisha wanamuziki kutoka nchi mbalimbali ambazo kihistoria zinahusishwa na barbara ya hariri . Rekodi zake hutolewa na lebo ya Sony Classical .

Yo-Yo Ma amepiga muziki wa filamu nyingi maarufu. Pia ametoa zaidi ya albamu 75, 15 zikiwa ni washindi wa Tuzo za Grammy.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]