Chi Zhuze

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Xi Guizi)
Wafiadini Wakatoliki wa China.

Chi Zhuze (pia: Xi Guizi; Dezhaoin, 1882 hivi - Dechao, mnamo Juni au Julai 1900) alikuwa mvulana mkatekumeni wa China aliyefia Ukristo wakati wa Uasi wa Waboksa. Hao walipofanya fujo, Chi alijitambulisha kama Mkristo akapigwa vibaya hadi kufa, akibatizwa hivyo katika damu yake [1].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 20 Julai[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.