WordPress

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wordpress ni programu ambayo inawasaidia wenye blogu kuweka makala katika blogu zao kwa urahisi. Imetengenezwa na PHP na MySQL. Programu hii ni ya bure yaani mtumiaji hahitaji kulipa chochote ili kuitumia. Huwa pia ni open source yaani kila mtu anaweza kuendeleza programu hii na kuiboresha zaidi. Kando na kutumika na wanablogu, wordpress pia hutumika na wenye jukwaa (forum) za kujadili mambo kadha wa kadha, wanaoweka picha za sanaa katika wovuti (media galleries) pamoja na wanaofanya mauzo kwa mitandao (ecommerce stores).

Historia ya Wordpress[hariri | hariri chanzo]

Wordpress hutumiwa na zaidi ya watu milioni sitini katika wavuti zao. Wordpress ilianzishwa mwakani 2003 na Matt Mullenweg na Mike Little. Imeidhinishwa na leseni ya GPLv2. Ili kufanya kazi, ni lazima wordpress iwekwe kwa seva ya wavuti. Kabla ya kubuniwa kwa wordpress, wenye wavuti iliwabidi wajue kutumia lugha za PHP na MySQL au HTML ili kuweza kupamba wavuti na blogu zao vile walivyokuwa wakitaka. Wordpress huwa na usanifu wa kutumia plugins ambavyo ni vipengele vinavyokusaidia kupamba wavuti yako na ifanye kazi unayotaka. Kando na plugin, pia huwa na template ili kwamba kazi yako tu ni kuweka makala yao kwa zile templates.

Sifa za Wordpress[hariri | hariri chanzo]

Unapoweka Wordpress kwa wavuti yako, utapatana na sifa hizi:

Theme[hariri | hariri chanzo]

Theme hutengeneza mandhari ya wavuti yako. Kuna wordpress themes nyingi za bure ambazo watengenezaji wameziweka ili uweze kutumia pia kulipa chochote. Vile vile, kuna themes amabzo hulipiwa na hutoweza kuzitumia bila kuzinunua. Kwa kawaida themes za bure huwa hazina mvuto mkubwa kwa wale wanaotembelea wavuti yako au pengine hazina matumizi mengi.

Unapotafuta theme ya wavuti yako, italingana na wavuti ni ya aina gani. Themes za sanaa zinazoonyesha picha au michoro huwa ni tofauti na zile za biashara ama zile za kusoma makala.

Plugins[hariri | hariri chanzo]

Plugins ni vipengele vinavyosaidia wavuti kufanya kazi unayotaka. Vile vile plugins huwa za bure au za kununuliwa. Kuziweka pia ni rahisi japo kila plugin huwa na masharti yake ya jinsi utakavyoiweka.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]