Nenda kwa yaliyomo

Winnie Mpanju-Shumbusho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Winnie Mpanju-Shumbusho ni Mtanzania na ni kiongozi wa Afya ya umma.

Mpaka tarehe 31 Desemba 2015 alifanya kazi kama Mkurugenzi msaidizi kitengo cha VVU/UKIMWI. TB, Malaria na magonjwa mengine ya kitropiki huko Geneva, Uswizi.

Kuanzia mwaka 2016 hadi 2019 alikuwa Mwenyekiti wa bodi ya kutokomeza ugonjwa wa malaria (RBM Pertnership to End Malara)[1].

Kabla ya kujiunga na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 1999, Dr. Mpanju-Shumbusho alikuwa Mkurugenzi mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini ambayo zamani ilijulikana kama jumuiya ya Afya ya kanda ya Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na afrika ya Kusini.

Mpanju-Shumbusho ni mwanzilishi, mjumbe wa bodi na anajitolea katika shirika la kilimo lisilokuwa la kifaida la AHEAD Inc. ambalo lilizinduliwa mwaka 1981 kwa lengo la kutoa msaada, msaada wa watu kwa watu, usaidizi kwa jamii maalumu za ndani ya Afrika na ndani ya miji ya ndani ya Marekani (USA). Pia ni mwanzilishi wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania na alifanya kazi kama mweka hazina na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho.

Mwaka 2019, alitunukiwa tuzo ya heshima ya Multsector.

Dr. Mpanju-Shumbusho ameolewa na ana watoto wawili.

  1. Zarocostas, John (Aprili 2018). "Winnie Mpanju-Shumbusho: leader in the fight against malaria". The Lancet. 391 (10130): 1566. doi:10.1016/S0140-6736(18)30894-8.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Winnie Mpanju-Shumbusho kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.