Nenda kwa yaliyomo

Wineaster Anderson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wineaster Anderson
Amezaliwa29 October 1974
UtaifaMtanzania
MhitimuChuo Kikuu cha Dar es Salaam [(Shahada ya Kwanza ya Biashara (B.Com 1999) na Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (MBA 2001)] na Chuo Kikuu cha Balearics (UIB) [Shahada ya Umahiri katika Uchumi wa Utalii na Mazingira (MTEE 2005), Shahada ya Uzamivu katika Uchumi wa Utalii na Mazingira (PhD TEE 2008)]
Kazi yakeProfesa wa Masoko na Usimamizi wa Biashara; Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma anayesimamia Mipango, Fedha na Utawala
Miaka ya kazi2001 Price Waterhouse Coopers, Mkaguzi; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 2001-2022

Wineaster Anderson (PhD) ni Profesa wa Masoko (Marketing) na kwa sasa, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala. Zamani alikuwa Amidi (dean) wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uhakiki na Uthibiti Ubora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam[1]. Ana Shahada ya Uzamivu (PhD) (2008) na Shahada ya Umahiri (2005) katika Uchumi wa Utalii na Mazingira (Tourism and Environmental Economics) na vile vile Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (MBA) (2001) na Shahada ya Kwanza (Bachellor of Commerce) Biashara (1999) katika Masoko. Wineaster Anderson alisoma katika Shule ya Sekondari ya Weruweru kidato cha kwanza hadi cha sita kuanzia 1989, wakati Shule ikiongozwa na Maria Josephine Kamm. Alisoma katika Shule ya Msingi Maring’a Chini iliyopo Mwika Kaskazini, Kilimanjaro kuanzia 1982 hadi 1988.

Anderson amefanya utafiti na kuchapisha kwa upana katika maeneo ya biashara ya kimataifa, utalii endelevu, kupunguza umaskini, jinsia na masoko.[2][3]

  • 2021: “Marketing Hall of Fame in Tanzania” [Tanzania Marketing Science Association]
  • 2019: “A Woman of Success 2019” [University of Dar es Salaam]
  • 2018: “Tanzania Women Champions in Tourism” [Africa Reconnect]
  • 2015: “Women of Achievement Award in Tanzania" [Life Time Achievement]
  • 2010: Highly Commended-African Management Research Fund [Emerald/ALCS]
  • 1999: Highly Commended Essay Writter for the EAC [The Konrad-Adenauer-Stiftung]
  1. https://www.researchgate.net/profile/Wineaster-Anderson
  2. "Wineaster Anderson". scholar.google.com. Iliwekwa mnamo 2023-11-15.
  3. "Wineaster Anderson | The University of Dodoma, Tanzania - Academia.edu". udom.academia.edu. Iliwekwa mnamo 2023-11-15.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wineaster Anderson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.