William Morris Carter

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

William Morris Carter (1873-1960) alikuwa mwanasheria wa Uingereza na msimamizi wa kikoloni. Alihudumu kama msajili na jaji nchini Kenya, Uganda na Tanganyika kati ya 1902 na 1924. Alijaribu bila mafanikio kutenganisha ardhi iliyoshikiliwa na Waafrika nchini Uganda ili yaweze kutumika kama mashamba ya Ulaya kwa kutumia vibarua . Aliongoza tume ya ardhi ya Rhodesia Kusini mwaka 1925 na Tume ya Ardhi ya Kenya ya 1932-1933, maeneo yote waliwafukuza Waafrika kutoka kwenye ardhi yao na kutenga maeneo hayo makubwa kwa ajili ya makazi ya wazungu pekee. Alihudumu katika Tume ya Kifalme ya Palestina (1936-1937).

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

William Morris Carter alizaliwa huko Canterbury, Uingereza mnamo 1873. Alisoma katika Shule ya Mfalme, Canterbury na Chuo Kikuu cha Oxford, kisha akajiunga na utawala wa kikoloni wa Uingereza.

Mwaka 1906 Jaji William Morris Carter alitoa ripoti kuhusu umiliki wa ardhi wa Buganda, na Septemba 1907 alitoa taarifa nyingine iliyohusu baadhi ya maeneo nje ya Buganda. Mnamo Machi 1907 kamati ya umiliki wa ardhi, ambayo Carter alikuwa mwanachama, iliwasilisha mapendekezo yake kwa serikali. Hata hivyo, wazo la kutengwa kwa ardhi kwa ajili ya wahamiaji wa Ulaya halikuzingatiwa vyema na gavana wa Uganda Henry Hesketh Bell kwa wakati huu.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu William Morris Carter kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.