Wikipedia Zero

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wikipedia Zero logo
Nchi ambako Wikipedia Zero ilipatikana mnamo 6 Septemba 2016.
Video kuhusu barua ya wanafunzi wa Afrika Kusini kuomba kuanzishwa kwa Wikipedia Zero nchini mwao.

Wikipedia Zero ilikuwa mradi wa taasisi ya Wikimedia Foundation iliyolenga kuwapa watumiaji wa simu za mkononi nafasi ya kutumia Wikipedia bure yaani bila gharama kupitia simu zao. [1][2]

Kazi ya mradi[hariri | hariri chanzo]

Mradi huu ulianzishwa mwaka 2012. [3]

Lengo lake ni kuomba kampuni za mawasiliano kufungua Wikipedia bila gharama kwa wateja wao.

Hadi Mei 2014 Wikipedia Zero ilifaulu kupata nafasi hii katika nchi 29 kwa ushirikiano na makampuni ya simu 33.

Wikipedia Zero katika Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Katika Afrika ya Mashariki ni Kenya (Orange, Airtel na Safaricom), Uganda (Orange) na Rwanda (MTN) ambako makampuni mbalimbali ya simu yalifungua nafasi hii kwa wateja wao. Kampuni ya Orange inaruhusu pia watumiaji wake wa Kongo-Kinshasa kushiriki.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wikipedia Zero ilianza nchini Malaysia Mei 2012.[4] Nchi za Thailand na Saudia zilifuata.

Nchini Afrika Kusini kampuni ya MTN ilikubali baada ya kupokea barua kutoka wanafunzi wa shule ya sekondari waliowahi kusikia kuhusu Wikipedia Zero nchini Kenya na kuomba makampuni ya simu ili wapewe nafasi hii ya kujisomea pia.

Mnamo Februari 2018, Wikimedia Foundation ilitangaza kuwa Wikipedia Zero itaachwa mwishoni mwa mwaka huo.[5][6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: