Wikipedia:Makala ya wiki/Charles Darwin
Charles Robert Darwin (12 Februari 1809 - 19 Aprili 1882) alikuwa mwanasayansi Mwingereza katika karne ya 19. Amekuwa mashuhuri kutokana na nadharia yake ya maendeleo ya uhai mageuko ya spishi. Nadharia hii yasema kuwa spishi zote za viumbehai vimetokana na spishi asilia zilizogeuka baada ya muda. Mageuko haya hufuata uteuzi asilia yaani viumbehai wanaolingana vizuri zaidi na mazingira wanaishi na kuzaa kushinda viumbehai wasiolingana nayo. Kwa njia hiyo tabia za viumbehai wanaofaa vizuri zaidi zinazidi kuendelezwa kwa sababu watoto wao hurithi tabia hizi. Lakini tabia za viumbehai wasiofaa sana zinaweza kutoweka kwa sababu wanakufa mapema na hawana watoto wengi wanaoendeleza tabia zao.
Alizaliwa mjini Shrewsbury (Uingereza) kama mtoto wa tano wa daktari Robert Darwin na Susannah Darwin (née Wedgwood). Baada ya kumaliza shule alijiunga na chuo kikuu cha Edinburgh (Uskoti) 1825 akajiandikisha katika idara ya tiba lakini hakupenda upasuaji. Alitumia muda mwngi kufuata kozi za biolojia, jiografia na jiolojia nje ya masomo ya tiba. Alifuatana mara nyingi na wataalamu walipofanya uchunguzi wa wanyama, mimea au mawe. ►Soma zaidi