Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Anthony Cruz (AZ)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Anthony Cruz
Taarifa za awali
AmezaliwaMachi 9, 1972
New york, Marekani
Miaka ya kazi1992 hadi sasa
StudioEMI, Noo Trybe, Virgin, Motown, Koch, Quiet Money
Ameshirikiana naThe Firm,Nas, Foxy Brown, Cormega, Nature

Anthony Cruz (anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii AZ; alizaliwa 9 Machi 1972) ni mwanamuziki wa Marekani anayetokea Brooklyn mjini New York.

Anafahamika kwa kuwa amekuwa mtu wa karibu na mwanamuziki Nas kwa kipindi kirefu na pia kuwa miongoni wa wanamuziki katika kikundi cha The Firm akiwa pamoja na Nas Foxy Brown, Cormega na Nature. Katika orodha ya wanamuziki pendwa wa hip hop wa muda wote iliyochapishwa katika mtandao wa About.com ilisema kuwa AZ alikuwa ni namba 1.

AZ kwa mara ya kwanza alijulikana kutokana na kuwepo katika albamu ya mwanamuziki Nas iliyoitwa Illmatic katika nyimbo iliyojulikana kama "Life's A Bitch". AZ, alijiunga na EMI na kuachia kibao chake kilichoitwa Doe or Die mnamo mwaka 1995. Wimbo wake wa "Sugar Hill" ulikkuwa ni wimbo wa mafanikio na kumfanya kushika nambari 25 katika orodha ya nyimbo za Bilbord 100. Mkataba wa AZ na EMI uliamishwa kwenda katika lebo dada za Noo Trybe Records na Virgin Records pale ambapo EMI ilivunjika.

Mnamo mwaka 1997, AZ alijiunga na kundi jipya, The Firm akiwa pamoja na Nas, Nature, na Foxy Brown na kuachia albamu yao kwa pamoja iliyojulikana kama "The Album". Mwaka uliofuata AZ alitoa albamu yake ya pili iliyojulikana kama Pieces of a Man. Albamu hiyo ilifanya vizuri lakini hakukuwa na wimbo hata mmoja wa kuweza kuizidi "Sugar Hill".

Baada ya albamu hii, AZ alijiunga na kundi la Motown na Universal Records na kutoa kibao cha 9 Lives na kufuatiwa na kingine kijulikanacho kama Aziatic. Wimbo wa "The Essence," aliomshirikisha Nas ulichaguliwa katika tuzo za 2003 Grammy Awards kama wimbo bora uliofanywa na kikundi.

Maisha ya awali

[hariri chanzo]

Cruz Alizaliwa Bedford–Stuyvesant, Brooklyn, New York, kutoka kwa mama aliyekuwa Mmarekani mweusi na baba ambaye alikuwa wa taifa la Dominica. Alikua katika nyumba ya ndugu yake ambako aliishi pamoja na mama yake na dada yake.

AZ alianza kuandika nyimbo akiwa na umri wa miaka 12. Katika miaka ya 1990 alikutana na mwanamuziki mdogo Nas, kutokea Queens. Nas alianza kurekodi albamu yake ya Illamatic na kumualika AZ kujiunga nae katika studio. AZ alionekana katika matangazo ya albamu hiyo na kuimba katika nyimbo iliyoitwa "Life's a Bitch". Baada ya albamu hiyo kuachiwa katika miaka ya 1994, EMI Records wakampa ofa AZ kujiunga na Kundi lao.

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wikipedia:Anthony Cruz (AZ) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.