Vulogu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vulogu (kwa Kiingereza: vlog) ni aina ya blogu ambayo huwa mbinu yake ya uwasilishaji wa jumbe ni kwa kutumia video. Kwa mapana, vulogu ni blogu ya video (video blog). Kwa wengi, video zao huwekwa kwa wavuti ya Youtube ambayo ndiyo iliyo na video nyingi sana.

Historia ya Vlogu[hariri | hariri chanzo]

Msanii Nelson Sullivan alijulikana kwa kurekodi kazi yake na kuiwasilisha kwa watu kwa kutumia vulogu. Kazi yake aliiweza kurekodi katika miji tofauti kama vile New York.

Vulogu za kisasa[hariri | hariri chanzo]

Vulogu zilipata umaarufu sana mwaka 2005. Leo, ni watu wengi walio na vulogu zinazowasilisha jumbe tofauti kutoka masomo ya kupika, hisabati, uchumi, malezi, urembo na hata afya njema ya mwili.

Unachohitaji ili kuwa na vulogu[hariri | hariri chanzo]

  • Hadhira ya kuwasilishia jumbe zako
  • Uzoefu wa kuweka video
  • Kamera nzuri ya kuchukua video pamoja na "vlogging tripod" ya kusaidia kuchukua video zako.