Nenda kwa yaliyomo

Vin Garbutt

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vin Garbutt mwaka 2010

Vincent Paul Garbutt (20 Novemba 1947 - 6 Juni 2017) [1] alikuwa mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za kitamaduni wa Uingereza.

Sehemu kubwa ya mkusanyiko wake wa nymbo ulijumuisha nyimbo za maandamano zinazoshughulikia mada kama vile "Matatizo" yaliyokuwa yakitokea huko Ireland Kaskazini (Welcome Home Howard Green, Troubles of Erin, To Find Their Ulster Peace), ukosefu wa ajira, na masuala ya kijamii. Ingawa mada ya nyimbo zake iliangazia masuala mbali mbali ya kisiasa na kijamii, ustadi wa Garbutt jukwaani, ucheshi na usimulizi wa hadithi kati ya nyimbo ulivuma sana katika hadhira yake na ambayo ilimfanya kujulikana sana.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]
Vin Garbutt akipumzika wakati wa ziara yake ya Australia, 1994

Garbutt alizaliwa huko Coral Street, South Bank, Middlesbrough, Uingereza, mtoto wa baba Mwingereza na mama wa Ireland. [2] Ingawa maonyesho yake ya kwanza ya moja kwa moja yalikuwa katika bendi ya muziki wa pop iitwayo "The Mystics", aligundua muziki wa kitamaduni akiwa bado shuleni na akaanza kutembelea na kutumbuiza katika Klabu ya Rifle katika mtaa wa Cannon, Middlesbrough, na baadaye katika klabu ya Eston Folk karibu na nyumbani kwake.  .

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
    • The Valley of Tees (1972)
    • The Young Tin Whistle Pest (live) (1974)
    • King Gooden (1976)
    • Eston California (1977)
    • Tossin' a Wobbler (1978)
    • Little Innocents (1983)
    • Shy Tot Pommy (1985) [live – Mount Isa, Queensland, Australia]
    • When The Tide Turns (1989)
    • The By-Pass Syndrome (1991)
    • Bandalised (1994)
    • Plugged! (1995) [live – Red Lion Folk Club, Birmingham, UK.]
    • When the Tide Turns Again (1998) [reissue of 1989 album with one additional track]
    • Word of Mouth (1999)
    • The Vin Garbutt Songbook Vol 1 (2003)
    • Persona ... Grata (2005)
    • Teesside Troubadour documentary feature & live DVD (2011)
    • Synthetic Hues (2014)
  1. "Folk legend Vin Garbutt died just weeks after major heart surgery". Gazette Live. Iliwekwa mnamo 6 Juni 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Vin Garbutt – biography". Vingarbutt.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-30. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)