Chuo Kikuu cha Witwatersrand
26°11′27″S 28°1′49″E / 26.19083°S 28.03028°E
Chuo Kikuu cha Witwatersrand | |
---|---|
Staff | 1 951 |
Wanafunzi | 24 381 |
Mahali | {{{mji}}} |
Tovuti | http://www.wits.ac.za/ |
Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg ni mojawapo ya vyuo vikuu bora vya Afrika Kusini lililoko katika maeneo ya kaskazini ya katikati mwa Johannesburg. Kinajulikana vizuri zaidi kama Wits University. Chuo hiki kina mizizi yake katika sekta ya madini, kama ilivyo Johannesburg na Witwatersrand kwa ujumla.
Mwaka wa 1959, sheria ya Extension of Education Act iliweka vikwazo kwa usajili wa wanafunzi weusi kwa karibu kipindi chote cha sera ya kibaguzi; hata hivyo, viongozi kadhaa weusi mashuhuri walihitimu kutoka chuo hiki. Kilimaliza ubaguzi tena punde tu kabla ya kukomeshwa kwa sera ya kibaguzi ya apartheid mwaka wa 1990. Baadhi ya wakosoaji wengi wa enzi ya kibaguzi, wa aidha asili ya kizungu au Kiafrika, walikuwa wakati moja wanafunzi na wahitimu wa chuo hiki.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Chuo kilianzishwa kama shule mjini Kimberley mwaka wa 1896 kama "South African School of Mines". Miaka minane baadaye, mnamo mwaka wa 1904 shule ilihamia Johannesburg na kubadili jina lake kwa "Transvaal Technical Institute". Ilibadilisha jina lake mwaka wa 1906 kuwa "Transvaal University College". Mnamo 1908 tawi la shule la Pretoria lilianzishwa, halafu mwaka wa 1910 shule tena iligeuza jina lake na kuwa "South African School of Mines and Technology". Hatimaye, mwaka 1922, shule ilipandishwa cheo na kuwa chuo kikuu kamili baada ya kukifanya Chuo kuwa "Chuo Kikuu cha Witwatersrand". Eneo la Milner Park, kaskazini-magharibi mwa Braamfontein lilitambuliwa kama makao ya kampasi mpya ya chuo kikuu, na ujenzi ulianza mwaka huo. Kulikuwa kuwe na vitivo sita vilivyotoa shahada ya digrii katika Chuo hiki: sanaa, sayansi, utabibu, uhandisi, sheria, na biashara.
Chuo kilipata kukua pakubwa baada ya kuidhinishwa kwake kama chuo kikuu, ongezeko kutoka wanafunzi 6,275 tu mwaka wa1963 hadi zaidi ya 16,400 mwaka wa 1985. Mwaka wa 1964, katika Maktaba ya Kitivo cha Tiba ilihamishwa hadi baraste ya Esselen Street, katika sehemu ya Hillbrow Johannesburg. Katika miaka ya 1960, chuo kilifungua shule nyingi mpya na majengo, na kutwaa pango la chokaa mawe lililo maarufu kwa vifaa vya kale linalopatikana Sterkfontein. Shule ya Uzamili ya Biashara ilianzishwa baadaye mwaka 1968 katika Parktown.
Shamba karibu na Sterkfontein liitwaalo Swartkrans lenye utajiri wa vifaa vya kale lilinunuliwa mwaka wa 1968, na haki za kulifukua zilipatikana kwa madhumuni ya kipalaontolojia Makapansgat, katika Jimbo la Limpopo. Mwaka uliofuata, makao ya Ernest Oppenheimer yalifunguliwa karibu na shule ya Biashara Parktown, na baadaye mwaka huo huo, idara za kliniki katika shule mpya ya Utabibu ilipofunguliwa. Mwaka wa 1976, Lawson's Corner iligeuzwa jina na kuitwa University Corner. Seneti House, jengo kuu la utawala la chuo kikuu, lilikamilika mwaka wa 1977. Chuo kikuu kilipata upanuzi mkubwa mwaka wa 1984, na kupata Milner Park showgrounds kutoka kwa Transvaal Agricultural Society, na kuifanya kampasi ya magharibi.
Mwaka wa 1984, jengo la Chama cha Migodi lilifunguliwa. Njia kubwa kwa jina la Amic Deck ilijengwa kuvukia barabara kuu ya De Villiers Graaff ambayo huigawanya kampasi mara mbili, ikiunganisha pande za mashariki na magharibi. Mwaka 2004, Chuo cha Elimu cha Johannesburg kilijumuishwa katika Wits kama kampasi ya elimu chini ya mpango wa elimu wa kitaifa wa mageuzi ya idara ya elimu katika Afrika Kusini.
Nafasi yake
[hariri | hariri chanzo]Mfumo wa THE- QS World University Rankings imeipa Wits nafasi ya 301 ulimwenguni kwa Shahada za kwanza.
Makampasi
[hariri | hariri chanzo]Chuo Kikuu kimegawanywa katika kampasi za taaluma tano. Kampasi ya Braamfontein (ambayo hutumika kama kampasi kuu ya usimamizi) imegawanywa katika kampasi za Mashariki na Magharibi na M1 (De Villiers Graaff Highway) na baraste ya Yale. Kampasi mzima Imepakana na barabara ya Empire (kaskazini), baraste ya Jan Smuts (Mashariki), barabara za Jorrissen na Enoch Sontonga (kusini) na ile ya Annet (magharibi). Kampasi ya kihistoria ya mashariki ndio makao ya vitivo vya sayansi na masomo ya kibinadamu, na vile vile Seneti na utawala wa Chuo Kikuu. Kampasi ya magharibi ni makao ya vitivo vya biashara na uhandisi. Kampasi kuu ndio makao ya makazi 6 yaani makazi ya Sunnyside na Jubilee (makazi ya wanafunzi wa kike), makao ya wanaume (makazi ya College na Dalrymple), Majumba ya Barnato, David Webster, West Campus Village na International House.
Katika kampasi ya Braamfontein kuna taasisi tatu za masomo, zote zikiwa Parktown. Kampasi ya Elimu ya Wits hujishughulisha na elimu, ambayo ni shule katika Kitivo cha Masomo ya Kibinadamu. Kampasi ya elimu inajivunia kuwa na makazi matatu ya wanafunzi wa kike; yaani Girton, Medhurst na Reith Hall. Mashariki ya kampasi ya elimu (upande wa pili wa barabara ya York), ndio makao ya Shule ya Udaktari ambayo ni makao makuu ya utawala wa Kitivo cha taaluma ya sayansi ya afya.
Magharibi ya kampasi ya elimu (upande wa pili wa Victoria Avenue) ndipo makao ya Shule ya Biashara ya Wits. Ni Shule ya biashara inayoongoza na inayoheshimika zaidi Afrika Kusini. Ndani ya mipaka ya shule ya biashara mna Majumba ya Ernest Oppenheimer (makao ya wanafunzi wa kiume) na pia Parktown Village I.
Mashariki ya kampasi ya elimu ni Wits Medical School, ambayo imehusishwa na moja wapo wa hospitali 4 za kufundisha - Charlotte Maxeke Johannesburg Academic Hospital.
Kuna vituo ambavyo si vya kitaaluma ingawa vinajulikana na Chuo Kikuu kama kampasi. Hivi ni Graduate Lodge, Campus Lodge, South Court na Kituo cha Braamfontein; zote zikiwa katika kampasi Kuu ya Braamfontein. Aidha kuna Parktown Village II na Knockando Halls (za wanaume) katika Parktown, na makao ya Essellen Street Hillbrow.
Vitivo na shule
[hariri | hariri chanzo]Chuo Kikuu kina vitivo vitano:
Biashara, sheria, na Usimamizi
[hariri | hariri chanzo]Kitivo hiki hutoa shahada mbalimbali, za kwanza na shahada ya Uzamili katika uhasibu, biashara, uchumi, usimamizi, na sheria. Kinajivunia kuwa na shule ya biashara inayoheshimika yaani Wits Business School, pamoja na shule ya kuhitimu kujitoa kwa umma na usimamizi wa maendeleo. Kitivo hiki hushiriki katika mpango wa WitsPlus, mpango wa ziada kwa wanafunzi.
- Biashara, sheria, na Usimamizi Ilihifadhiwa 4 Aprili 2011 kwenye Wayback Machine.
Uhandisi na Ujenzi
[hariri | hariri chanzo]- Kitivo cha Uhandisi na Ujenzi Ilihifadhiwa 29 Machi 2010 kwenye Wayback Machine.
Sayanzi za Afya
[hariri | hariri chanzo]- Sayansi za Afya Ilihifadhiwa 15 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine.
Masomo ya Kibinadamu
[hariri | hariri chanzo]Hiki kina shule za Sanaa, Elimu, Sayansi, Fasihi na Masomo ya Lugha miongoni mwa wengine.
Sayansi
[hariri | hariri chanzo]- Sayansi Ilihifadhiwa 13 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine.
Majengo na vivutio katika kampasi
[hariri | hariri chanzo]- Kumbukumbu za kitaifa : Dias Cross na Great Hall (zilizoko mashariki ya kampasi ya Braamfontein) zimepewa staha ya kitaifa.
- Maonyesho ya Sanaa0}: Kuna maonyesho mawili ya umma ya sanaa yaani Maonyesho ya sanaa ya Gertrude Posel na ya Studio, yote yako katika Jumba la Seneti. Maonyesho ya sanaa ya Studio yanajulikana kwa kuwa na mkusanyiko bora zaidi wa shanga za kiafrika duniani.
- Sanaa miamba: Mkusanyiko wa Roberts-Pager wa nakala za sanaa miamba ya Watu walioishi mwituni, ziko katika jengo la Van Riet Lowe kampasi ya mashariki.
- Makavazi: Chuo kina takriban makavazi kumi na nne. Hizi ni pamoja na Makavazi ya Adler (ya historia ya dawa), ya Palayontolojia na makavazi ya kipekee ya Jiolojia mjini Gauteng. Maonyesho yanajumuisha mkusanyiko mkubwa wa vifaa kama vile Fuvu la Taung, magofu ya dinosaur na vipepeo.
- Kitovu cha mwanadamu: Hifadhi ya kimataifa iliyoko magharibi wa Johannesburg. Mapango ya Swartkrans na Sterkfontein yanajulikana kote duniani kama baadhi ya vyanzo vikubwa vya magofu ya hominidi duniani.
- Usayaria wa Johannesburg: [1] uliofunguliwa mwaka wa 1960, ndio usayaria wa kwanza kamili barani Afrika, na wa pili Kusini mwa ulimwengu.
Wanafunzi wa Zamani na wasomi mashuhuri
[hariri | hariri chanzo]Walotuzwa Tuzo ya Nobel
[hariri | hariri chanzo]- Aaron Klug, 1982 Tuzo ya Nobel ya Kemia
- Nadine Gordimer, 1991 Tuzo ya Nobel ya fasihi
- Nelson Mandela, 1993 Tuzo ya Amani ya Nobel
- Sydney Brenner, 2002 Tuzo ya Nobel ya Utabibu
Vitabu kuhusu chuo hiki
[hariri | hariri chanzo]- The Golden Jubilee of the University of Witwatersrand 1972 ISBN 0-85494-188-6 (Jubilee Committee, University of Witwatersrand Press)
- Wits: The Early Years: a History of the University of Witwatersrand Johannesburg and its Precursors 1896 - 1936 1982 Bruce Murray ISBN 0-85494-709-4 (University of Witwatersrand Press)
- Wits Sport: An Illustrated History at the University of Witwatersrand 1989 Jonty Winch ISBN 0-620-13806-8 (Windsor)
- Wits: A University in the Apartheid Era 1996 Mervyn SHEAR ISBN 1-86814-302-3 (University of Witwatersrand Press)
- Wits: The "Open Years": A History of the University of the Witwatersrand, Johannesburg, 1997 Bruce 1939-1959 Murray ISBN 1-86814-314-7 (University of Witwatersrand Press)
- A Vice-Chancellor Remembers: the Memoirs of Professor GR Bozzoli 1995 Guerino Bozzoli ISBN 0-620-19369-7 (Alphaprint)
- Wits Library: a Centenary History Reuben 1998 Musiker & Naomi Musiker ISBN 0-620-22754-0 (Scarecrow Books)