United African Alliance Community Center

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

United African Alliance Community Center (kwa kifupi UAACC) ni shirika lisilo la kiserikali lililopo mkoani Arusha [1]. Shirika hilo lilianzishwa mwaka 1991 [2] na Pete O'Neal pamoja na mke wake Charlotte Hill O'Neal kwa malengo ya kuwasaidia watoto pamoja kuendeleza utamaduni.

Shirika hilo linapatikana katika wilaya ya Arumeru, nje kidogo ya mji mdogo wa Usa River na wanafunzi ndani ya kituo hiki hujifunza sanaa, kompyuta, ufundi pamoja na lugha ya Kiingereza na elimu hizo hutolewa bila ya malipo [3]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu United African Alliance Community Center kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.