Pete O'Neal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Felix Lindsey "Pete" O'Neal, Jr. (alizaliwa 1940) alikuwa mwenyekiti wa chama cha Black Panther Party cha mji wa Kansas nchini Marekani mwaka 1960 huku akifanya shughuli nyingi za kijamii kama kusaidia watoto wa mitaani katika mji huo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

O'Neal aliingia katika mgogoro na walimu wake wakati akiwa elimu ya juu ya upili na kulazimika kuacha masomo yake na kujiunga na jeshi akifuata nyayo za baba yake.

Baada ya kumaliza kuhudumu katika jeshi alihamia katika jiji la Calfonia na mwaka 1959h alikamatwa kwa makosa ya wizi na kuhukumiwa jela miezi tisa lakini alitoroka baada ya kukaa humo kwa muda wa miezi mitatu na kukimbilia katika mji wa Kansas na mwaka 1961 alikamatwa tena na kurejeshwa katika jiji la Kalifonia kumalizia hukumu yake iliyobakia .[1]

Mnamo tarehe 30 Oktoba mwaka 1969 alikamatwa tena kwa makosa ya kusafirisha silaha na mwaka 1970 alihukumiwa jela miaka minne, lakini alitorokea nchini Aljeria na kisha kukimbilia nchi Tanzania baada ya mwalimu Julius Nyerere kuvutiwa na sera zake za uafrika na kumruhusu kuishi nchini humo ambako anaishi hadi sasa.

Peter pamoja na mke wake Charlotte Hill O'Neal, ni waanzilishi wa asasi na kituo cha United African Alliance Community Center (UAACC) kilichopo eneo la Embasenyi wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

UAACC ni kituo kinachoshughulika kufunza watoto hasa katika masuala ya sanaa. filamu. muziki lugha ya Kiingereza, Kompyuta pamoja na mambo mengine.

Kituo hiki kimekuwa kikitembelewa na watu maarufu pamoja na wanasiasa mbalimbali na huduma za mabweni zinapatikana katika kituo hiko, huku vijana na watu mbalimbali hasa wanaozunguka kituo hicho wakipata fursa ya ajira.

Familia ya O'Neal's bado inaishi katika jiji la Kansas na Peter ni binamu wa mwakilishi wa Marekani Emmanuel Cleaver, na tangu mwaka 1991 Eammanuel amekuwa akimuombea Pater msamaha kwa maraisi tangu Bill Clinton na Barack Obama na wote walikataa kutoa msamaha kwa Peter .[2][3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Pete O’Neal – Profiles in Kansas City Activism" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2021-01-12. 
  2. McKinley Jr, James C.. "A Black Panther's Mellow Exile: Farming in Africa", 23 November 1997. 
  3. New pardon push for Kansas City Black Panther founder Pete O'Neal living in exile in Africa, KSHB, Andy Alcock, April 5, 2016. Retrieved 6 November 2016.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pete O'Neal kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.