Ungamo la Augsburg
Mandhari
Ungamo la Augsburg ni mafundisho yaliyotungwa mwaka 1530 na wafuasi wa Martin Luther walipodaiwa kujieleza mbele ya Bunge la Dola Takatifu la Kiroma ili kurudisha umoja wa Kanisa[1].
Lengo lake lilikuwa kuendeleza matengenezo ya Kiprotestanti, lakini pia kudumisha umoja huo.
Katika sehemu ya kwanza (1-21) linafafanua mafundisho ya Kilutheri namna ya kuonyesha kwamba hayapingani na yale ya «Kanisa Katoliki au ya Kanisa la Roma».
Sehemu ya pili inazungumzia mabadiliko yaliyoanzishwa na watengenezaji ili kurekebisha mambo kadhaa yaliyotazamwa kama «maovu» (22-28), ikieleza haja ya mabadiliko hayo.
Ungamo hilo ni thibitisho tosha la nia ya Walutheri wa kwanza ya kubaki ndani ya Kanisa pekee linaloonekana.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ungamo la Augsburg kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |