Ufuoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ndani ya ufuoni wa kisasa; milango hufungua sehemu baridi za kuwekea maiti.

Ufuoni (kutoka kitenzi kufua; pia: makafani; kwa Kiingereza: mortuary) ni mahali, chumba au jengo la kuosha na kuhifadhi maiti kwa muda hadi yafanyike mazishi.

Zinapatikana katika hospitali na pia makaburini mwa miji mikubwa.

Kusudi la kuhifadhi maiti kwa muda ni pamoja na

  • kufanya utafiti wa kitiba kuhusu sababu za kifo
  • kutunza maiti aliyeokotwa au kupatikana mahali pa ajali hadi kuhakikisha marehemu alikuwa nani na kuwasiliana na ndugu zake
  • kupata muda wa usafiri wa ndugu walio mbali na mahali pa mazishi waweze kufika
  • katika nchi kadhaa muda unahitajika hadi kupata nafasi kwenye makaburi ya miji mikubwa, hasa kama maiti anachomwa

Kwa kawaida kuna mitambo ya kupoza miili ili kuzuia au kuchelewesha mchakato wa kuoza kwa maiti.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ufuoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.