Ufugaji wa samaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtu akiwa ndani ya bwawa lake la samaki.
Huu ni mfano wa samaki bora.

Ufugaji ni kitendo cha kufuga samaki, ndege au wanyama. Humu tutazungumzia kuhusu ufugaji wa samaki. Kwanza samaki wanapaswa kuwa bora na pia wana faida na hasara mbalimbali katika kufuga.

Ubora wa samaki[hariri | hariri chanzo]

Ukubwa, mwonekano na ladha ni muhimu vikazingatiwa pindi samaki wawapo bwawani hadi kuvuna. Wakati wa kuvuna hakikisha samaki wako hawapati majeraha na pia hawatumii nguvu nyingi ili wasiharibike mapema.

Faida za samaki[hariri | hariri chanzo]

•Hutupatia fedha.

•Hutupatia kitoweo.

•Hutufanya kujuana na watu mbalimbali n.k.

Changamoto zinazoathiri ufugaji wa samaki[hariri | hariri chanzo]

• Ukosefu wa mbegu bora na za kutosha.

• Kukosekana kwa wataalamu wa kutosha katika kutoa huduma za ugani hasa vijijini.

• Kukosekana kwa masoko ya uhakika (hasa kwa upande wa kambale).

Magonjwa[hariri | hariri chanzo]

Ufugaji wa samaki huusisha kutoa mbegu sehemu moja hadi nyingine hivyo kama hakutakuwa na umakini wa kutosha basi magonjwa yanaweza kuenezwa katika maji ya asili. Kwa maana hiyo, ni muhimu kuchunguza samaki wageni kabla ya kuwaweka bwawani.

Maji[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida ufugaji unahitaji kubadilisha maji na pia hata kutoa maji yote bwawani wakati wa kuvuna samaki. Kwa maana hiyo, kama maji yataachiwa moja kwa moja kwenda kwenye mazingira au kwenda kwenye maji ya asili yatasababisha uharibifu.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ufugaji wa samaki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.