Uchumi wa buluu
Uchumi wa buluu ni matumizi sahihi ya rasilimali zipatikanazo majini ili kukuza uchumi na uboreshaji wa maisha huku mfumo wa ikolojia ya bahari ukihifadhiwa.[1]
Rasilimali hizo zinajumuisha zote zipatikanazo katika maji safi na bahari, pamoja na ukanda wa pwani, maziwa, mito na maji chini ya ardhi.[2]
Sekta kuu za uchumi wa bluu ni sekta za jadi ambazo ni uvuvi, ufugaji wa samaki, utalii, usafiri na bandari pamoja na sekta zinazoibuka kama vile nishati mbadala na uchimbaji wa madini wa bahari kuu[3].
Historia
[hariri | hariri chanzo]Wazo la uchumi wa bluu lilibuniwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Rio+20 juu ya maendeleo endelevu, uliofanyika Rio de Janeiro mnamo Juni 2012. Wakati wa mchakato wa maandalizi ya Rio+20, nchi zilizo na ukanda wa pwani zilikuwa na wasiwasi kuhusu mwelekeo wa uchumi wa kijani kibichi na matumizi yake kwao, hivyo Taarifa thabiti ziliwasilishwa na kuunga mkono dhana ya "uchumi wa bluu" ili kushughulikia hali za mataifa haya .[4] Dhana ya uchumi imewasilishwa baadaye katika vikao vingi na inatazamwa kama mfano mbadala wa kiuchumi kwa maendeleo endelevu.[5]
Ufafanuzi
[hariri | hariri chanzo]kulingana na Benki ya Dunia uchumi wa bluu ni matumizi enedelevu ya rasilimali za bahari kwa ili kukuza uchumi, maisha bora, na ajiira huku tukihifadhi afya ya mfumo wa ikolojia ya bahari.[6]
Tume ya ulaya inaifafanua kama "" shughuli zote za kiuchumi zinazousiana na baharina pwani"".[7]
Jumuiya ya Madola inachukulia uchumi wa bluu kama ""dhana iliyoibuka ambayo inahimiza usimamizi bora wa rasilimali zutu za bahari"", uchumi wa bluu unaenda zaidi ya matazamio kuwa bahari ni moya ya vyanzo vya ukuzaji wa uchumi.[8]
Conservation Internation inaongeza kuwa "uchumi wa bluu pia unajumuisha faida za kiuchumi ambazo haziwezi kuuzwa, kama vile hifadhi ya kaboni, ulinzi wa pwani, maadili ya kitamaduni na bioanuwai."[9]
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni alifafanua Uchumi wa Bluu kama uchumi "unaojumuisha sekta mbalimbali za kiuchumi na sera zinazohusiana, ambazo kwa pamoja huamua kama matumizi ya rasilimali za bahari ni endelevu. Changamoto muhimu ya uchumi wa bluu ni kuelewa na kusimamia vyema masuala ya uendelevu wa bahari, kuanzia uvuvi endelevu hadi afya ya mfumo ikolojia hadi kuzuia uchafuzi wa mazingira Pili, uchumi wa bluu unatupa changamoto kutambua kwamba usimamizi endelevu wa rasilimali za bahari utahitaji ushirikiano katika mipaka na sekta mbalimbali kupitia ubia mbalimbali, na kwa kiwango ambacho halijafanikiwa hapo awali. Umoja wa Mataifa unabainisha kuwa Uchumi wa Bluu utasaidia katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, ambapo lengo moja, 14, ni "maisha chini ya maji".
Uwezo
[hariri | hariri chanzo]Kando na shughuli za jadi za baharini kama vile uvuvi, utalii na usafiri wa baharini, uchumi wa bluu unajumuisha viwanda vinavyoibukia ikiwa ni pamoja na nishati mbadala, ufugaji wa samaki, shughuli za uchimbaji wa baharini na bioteknolojia ya baharini na uchunguzi wa viumbe. hai[10] Uchumi wa bluu pia unaambatanisha huduma za mfumo ikolojia wa bahari ambazo hazipo sokoni lakini hutoa mchango mkubwa kwa shughuli za kiuchumi na za kibinadamu. Zinajumuisha uondoaji wa kaboni, ulinzi wa pwani, utupaji wa taka, na uwepo wa bioanuwai.[11]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.un.org/regularprocess/sites/www.un.org.regularprocess/files/rok_part_2.pdf
- ↑ https://www.eac.int/environment/aquatic-ecosystems/blue-economy ilitazamwa 2024-16-05.
- ↑ https://www.uneca.org/blue-economy#:~:text=The%20main%20sectors%20of%20the,energy%20and%20deep%20sea%20mining.ilitazamwa mnamo 2014-16-05
- ↑ https://www.col.org/news/the-blue-economy-origin-and-concept/
- ↑ https://www.col.org/news/the-blue-economy-origin-and-concept/
- ↑ https://www.un.org/regularprocess/sites/www.un.org.regularprocess/files/rok_part_2.pdf ilitazamwa mnamo 2024-16-05
- ↑ https://op.europa.eu/en/publication-detail/-/publication/79299d10-8a35-11e8-ac6a-01aa75ed71a1
- ↑ https://web.archive.org/web/20181019231234/http://thecommonwealth.org/blue-economy ilitazamwa mnamo 2024-16-05
- ↑ https://www.conservation.org/blog/what-on-earth-is-the-blue-economy/?gclid=Cj0KCQjwl9zdBRDgARIsAL5Nyn3xGXHsApcgFjjO6CvN0Zg602NYYuJw2LPvqa_nDpKKxPtNDJWQxLYaAvSLEALw_wcB
- ↑ https://openknowledge.worldbank.org/bitstream/handle/10986/26843/115545.pdf?sequence=1&isAllowed=y
- ↑ https://openknowledge.worldbank.org/bitstream/handle/10986/26843/115545.pdf?sequence=1&isAllowed=y