Nenda kwa yaliyomo

Ubebaji Mke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ubebaji Mke (Kifini: eukonkanto au akankanto, Kiestonia: naisekandmine, Kiswidi: kärringkånk, Kiingereza: Wife-Carrying) ni mashindano ambayo washindani wa kiume hukimbia katika njia maalum yenye vikwazo zaidi wakati kila mmoja amembeba mwenzake wa kike. Mchezo huo ulianzishwa huko Sonkajärvi, nchini Ufini.

Aina kadhaa za kubeba zinaweza kutumika: ubebaji juu ya mabega, au mtindo wa Kiestonia (mke anakuwa kichwa chini na miguu juu ya shingo na mabega ya mwanaume).[1][2][3]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ubebaji Mke ilitokea nchini Ufini. Hadithi zimepitishwa kwa mtu anayeitwa Herkko Rosvo-Ronkainen (ajulikanaye kama Ronkainen the ʻRobber).[4] Mtu huyu alichukuliwa kama mnyang'anyi mwishoni mwa miaka ya 1800, aliishi msituni, na alikimbia na kundi lake la wezi wakisababisha madhara vijijini. Kutoka na yale yaliyopatikana, kuna maoni matatu juu ya kwanini / jinsi mchezo huu ulivumbuliwa. Kwanza, kwamba Rosvo-Ronkainen na wezi wake walituhumiwa kwa kuiba chakula na kuwateka wanawake kutoka vijiji katika eneo alilokuwa akiishi, kisha kuwabeba wanawake hawa migongoni wanapokimbia. Pendekezo la pili ni kwamba vijana wangeenda kwenye vijiji jirani, na kuwateka wanawake na kuwaoa kwa nguvu na mara nyingi wanawake hao ni wale ambao walikuwa tayari wamekwisha kuolewa. Vijana hawa pia waliwabeba hao wanawake migongoni: hii ilijulikana kama "mazoea ya kuiba wanawake. Mwishowe, ni wazo kwamba Rosvo-Ronkainen aliwafundisha wezi wake kuwa "wepesi na hodari" kwa kubeba mifuko mikubwa mizito migongoni mwao, ambayo ilipelekea kuvumbuliwa kwa mchezo huu[2].[5]

Ubebaji Mke ni mashindano ambayo yamefanyika Australia, Marekani, Hong Kong, Uhindi, Ujerumani, Uingereza na maeneo mengine ya ulimwengu kando na Ufini na Uswidi wa karibu na Estonia na Latvia, na mchezo huo una kitengo katika Kitabu cha kumbukumbu cha Guinness.[6][7][8]

Sheria za Mchezo

[hariri | hariri chanzo]

Mashindano ya asili yalifanyika katika eneo lenye miamba, lenye mawe na uzio na vijito, lakini baadae likabadilishwa ili kuendana na hali za kisasa. Sasa kuna mchanga badala ya miamba na mawe, uzio, na eneo lililojazwa maji (dimbwi). Zifuatazo ni sheria zilizowekwa na Kamati ya kimataifa ya mashindano ya Ubebaji Mke.

  • Urefu wa njia rasmi ni mita 253.
  • Njia hiyo ina vizuizi viwili kavu na kikwazo cha maji chenye kina cha urefu wa karibu mita moja.
  • Mke wa kubebwa anaweza kuwa wako mwenyewe, au wa jirani, au unaweza kuwa umemkuta katika mashindano; lazima, hata hivyo, awe na zaidi ya umri wa miaka 17.
  • Uzito wa chini wa mke kubeba ni kilo 49. Ikiwa ana uzito chini ya kilo 49, atabebeshwa begi lililo na uzito wa ziada ili kuleta mzigo wote wa kubeba hadi kilo 49.
  • Washiriki wote lazima wafurahie.
  • Vifaa pekee vinavyoruhusiwa ni mkanda unaovaliwa na mbebaji na kofia ya usalama iliyovaliwa na waliobeba.
  • Washiriki hukimbia mbio jozi mbili kwa wakati, kwa hivyo kila joto ni mashindano yenyewe.
  • Kila mshiriki hujali usalama wake na, ikionekana ni muhimu awe na bima.
  • Washiriki wanapaswa kuzingatia maagizo yaliyotolewa na waandaaji wa shindano.
  • Kuna kitengo kimoja tu katika Mashindano ya Dunia, na mshindi ni wenzi ambao wanamaliza kozi hiyo kwa muda mfupi zaidi.
  • Pia, wenzi wenye kuonyesha burudani zaidi, mavazi bora, na mbebaji hodari watapewa tuzo maalum.

Wakati sheria za Kimataifa ni msingi wa mashindano yote, sheria na zawadi zinatofautiana kwa kila mashindano.

Mashindano ya Dunia ya Ubebaji MKe yamekuwa yakifanyika kila mwaka huko Sonkajärvi, nchini Ufini, tangu 1992 (ambapo tuzo ni bia kulingana na uzito wa mke).[9][10]

Mabingwa wa Dunia

[hariri | hariri chanzo]
  • 2019 - Vytautas Kirkliauskas (Lithuania) na Neringa Kirkliauskiene (Lithuania), Sekunde 66.7 .
  • 2018 - Vytautas Kirkliauskas (Lithuania) na Neringa Kirkliauskiene (Lithuania), Sekunde 65.1.
  • 2017 – Taisto Miettinen (Finland) na Kristiina Haapanen (Finland), Sekunde 68.6.
  • 2016 – Dmitry Sagal (Russia) na Anastasia Loginova (Russia), Sekunde 62.7.
  • 2015 – Ville Parviainen (Finland) na Sari Viljanen (Finland), Sekunde 62.7.
  • 2014 – Ville Parviainen (Finland) na Janette Oksman (Finland), sekunde 63.7.
  • 2013 – Taisto Miettinen (Finland) na Kristiina Haapanen (Finland), Sekunde 65.0.[11]
  • 2012 – Taisto Miettinen (Finland) na Kristiina Haapanen (Finland), Sekunde 61.2.
  • 2011 – Taisto Miettinen (Finland) na Kristiina Haapanen (Finland), Sekunde 60.7.[12]
  • 2010 – Taisto Miettinen (Finland) na Kristiina Haapanen (Finland), Sekunde 64.9.
  • 2009 – Taisto Miettinen (Finland) na Kristiina Haapanen (Finland), Sekunde 62.0.
  • 2008 – Alar Voogla (Estonia) na Kirsti Viltrop (Estonia), Sekunde 61.9.[13]
  • 2007 – Madis Uusorg (Estonia) na Inga Klauso (Estonia), Sekunde 61.7.[14]
  • 2006 – Margo Uusorg (Estonia) na Sandra Kullas (Estonia), Sekunde 56.9.[15]
  • 2005 – Margo Uusorg (Estonia) na Egle Soll (Estonia), Sekunde 59.1.[16]
  • 2004 – Madis Uusorg (Estonia) na Inga Klauso (Estonia), Sekunde 65.3.[17]
  • 2003 – Margo Uusorg (Estonia) na Egle Soll (Estonia), Sekunde 60.7.[18]
  • 2002 – Meelis Tammre (Estonia) na Anne Zillberberg (Estonia), Sekunde 63.8.
  • 2001 – Margo Uusorg (Estonia) na Birgit Ulrich (Estonia), Sekunde 55.6.
  • 2000 – Margo Uusorg (Estonia) na Birgit Ulrich (Estonia),[19] Sekunde 55.5.
  • 1999 – Imre Ambos (Estonia) na Annela Ojaste (Estonia), Sekunde 64.5.
  • 1998 – Imre Ambos (Estonia) na Annela Ojaste (Estonia), Sekunde 69.2.[20]
  • 1997 – Jouni Jussila (Finland) na Tiina Jussila (Finland), Sekunde 65.0.[21]

Australia

[hariri | hariri chanzo]

Australian Wife Carrying Championships have been held annually since 2005.

Amerika ya kaskazini

[hariri | hariri chanzo]

Mashindano ya Kubeba Mke wa Amerika Kaskazini hufanyika kila mwaka tangu 1999 kwenye Juma la Siku ya Columbus mwezi Oktoba katika hotel ya Sunday River Ski Resort Newry, Maine.

  • 2019 – Washindi: Olivia na Jerome Roehm (Delaware)

Uingereza

[hariri | hariri chanzo]

Mchezo wa Ubebaji Mke Uingereza ulianzishwa mnamo mwaka 2008, ingawaje mchezo unadasadikika kufanywa kwa msaada kutoka kwa binamu zetu wa Scandinavia" kwa karibu miaka 300 kutoka 793AD wakati wavamizi wa Viking walipovamia vijiji na kuteka nyara wake.[24]

  • 2008 - Joel Hicks akimbeba Wendy Cook
  • 2009 - Matt Evans akimbeba Jatinder Gill (zawadi yao ilikuwa ni ujazo wa bia kilingana na uzito wao kwa pamoja - Kilo 120)
  • 2010 - John Lund
  • 2011 - Sam Trowbridge Akimbeba Nathalie
  • 2012 - Tom Wilmot akimbeba Kirsty Wilmot
  • 2013 - Mike Witko akimmbeba Lindsey Finn (Mike alisonga mbele na alishika nafasi ya 3 akimbeba Hattie Archer kwenye mashindano ya dunia nchii Ufini)
  • 2014 - Rich Blake Smith Akimbeba Anna
  • 2015 - Jonathon Schwochert akimbeba Charlotte Xiong (mashindano haya yalimshuhudia pia Joel Hicks akimbeba "Tiny Tina" rafiki wa kiume)
  • 2016 - Jonathan Schwochert akimbeba Charlotte Xiong (shindano hili lilimshuhudia Joel Hicks akibeba wake wawili lakini akamaliza wa mwisho)
  • 2017 - Jack McKendrick akimbeba Kirsty Jones
  • 2018 - Chris Hepworth akimbeba Tanisha Prince[25]
  • 2019 - Chris Hepworth akimbeba Tanisha Prince

Marekani

[hariri | hariri chanzo]

Fainali ya Amerika inafanyika wikendi ya pili ya Julai huko Menahga Minnesota (MN-St. Urho Wife Carry for Charity Challenge). Mashindano makubwa ya kubeba mke pia hufanyika Monona, Wisconsin, Minocqua, Wisconsin na Marquette, Michigan.

Ecorun India, jamii ya kuleta mwamko kuhusu mazingira waliandaa masindano ya Ubebaji Mke huko Thiruvananthapuram, Kerala, India, Asia mnamo tarehe 1 Januari 2011. Hafla hiyo inaitwa "Bhaaryaasametham" iliyotafsiriwa kama "na mke wako" katika Kimalayalam, lugha ya asili. Jamii inapanga kufanya hafla kama hizo kila mwaka nchini India. Ubebaji Mke Asia pia huitwa matukinina.Sinema ya kihindi inayoitwa Dum Laga Ke Haisha ilikuwa na "shindano la Ubebaji Mke" nyuma ya pazia.

Katika utamaduni maarufu

[hariri | hariri chanzo]
  • Mabingwa wa Amerika Kaskazini Ehrin na Aprili Armstrong walionyeshwa kama wageni waalikwa kwenye kipindi cha msimu wa kwanza wa revival of I've Got a Secret ya GSN.
  • Watangazaji wa BBC Mike Bushell na Steph McGovern walibadilisha majukumu yao wakati walishiriki mashindano ya kila mwaka ya Ubebaji Mke huko Uingereza mnamo 2013. Mtangazaji huyo wa kiume alisema hii ilikuwa ya kwanza.[26]
  • Margo Uusorg na Sandra Kullas wanashikilia rekodi ya ulimwengu wakati wa mashindano haya, wakimaliza njia ya mita 253.5 kwa sekunde 56.9 mnamo mwaka 2006[27]
  • Wahusika wakuu katika filamu ya Baba wa Mwaka wa 2018 waliingia na kushinda shindano la Ubebaji Mke

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. "What is Wife-Carrying?". Mental Itch (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  2. 2.0 2.1 "Wife Carrying | Cultures and Customs". sites.psu.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-11. Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  3. "Wife Carrying Official Rules and History" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  4. "Wife-carrying is a thing. This man and woman are world champs". South China Morning Post (kwa Kiingereza). 2018-07-08. Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  5. "Wife Carrying Is the Latest Strength Sport for Couples". BarBend (kwa American English). 2016-11-16. Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  6. "The Strange Sport of Wife Carrying | bettor.com". web.archive.org. 2011-02-19. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-02-19. Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  7. "Wife Carrying World Championship". Funny Jokes (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  8. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-01. Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  9. Jurvetson, Steve (2004-09-29), World “Wife Carry” Championships, iliwekwa mnamo 2021-03-17
  10. Cady Herring. "Plantation couple win beer, silver medal at Wife Carrying World Championships". sun-sentinel.com. Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  11. The Daily Telegraph, 10 July 2013, Finland hosts annual wife-carrying world championships Archived 9 Agosti 2020 at the Wayback Machine., Imewekwa mnamo 17/03/2021.
  12. "Wife-carrying team defends title", Melbourne: The Age, 2011-07-03. 
  13. "Wives in Finland worth their weight in beer". Canada.com. 2008-07-06. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-01-08. Iliwekwa mnamo 2010-07-05. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)
  14. "Estonia dominates wife-carrying championships", triplem.com.au, July 9, 2007. 
  15. "Estonians reign at wife-carrying championships", ABC News Online, 2006-07-02. 
  16. "Estonians snatch world wife-carrying title again", ABC News Online, 2005-07-03. 
  17. "Estonian carries 'wife' to glory", BBC News, 2004-07-04. 
  18. "Estonians romp home in wife-carrying contest". Cape Times. 2003-07-07. Iliwekwa mnamo 2010-07-11.
  19. "Estonia's clean sweep at wife-carrying", BBC News, 2000-07-02. 
  20. Huuhtanen, Matti. "Estonians take double victory in international wife carrying contest", Highbeam.com, 1998-07-04. Retrieved on 2021-03-17. Archived from the original on 2012-11-04. 
  21. "Finn carries the day – and his wife – in unique race", 1997-07-06. 
  22. "Estonia dominates wife-carrying championships", triplem.com.au, July 9, 2007. 
  23. 23.0 23.1 "Wife carrying makes its mark in Australia", news.com.au, News Limited, April 11, 2008. Retrieved on 2021-03-17. Archived from the original on 2011-01-19. 
  24. "The UK Wife Carrying Race". trionium.com. Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
  25. "UK wife-carrying contest takes place in Dorking". BBC. Aprili 8, 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  26. "BBC pair swap roles for 'wife carrying' race", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), iliwekwa mnamo 2021-03-17
  27. Guinness world records 2014. Internet Archive. [England] : Guinness World Records Limited. 2013. ISBN 978-1-908843-35-7.{{cite book}}: CS1 maint: others (link)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Ubebaji Mke kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.