Tuzo za muziki MTV Africa 2021

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hafla ya utoaji wa Tuzo za muziki za MTV Africa 2021 iliyopangwa kufanyika Kampala, Uganda ilighairishwa. Hafla hizo pia zingeonyeshwa kidunia katika nchi 180 kupitia kituo cha runinga cha MTV Base na MTV kwa mara ya kwanza kwa mujibu wa Paul Grein wa Billboard[1]. Hafla hizo zitatangazwa na DJ khaled akiwepo jiji la Miami[2]. Hafla hizo za tano zingetumbuizwa na wasanii maarufu Africa kama Wizkid, Diamond Platnumz, Khaligraph Jones, Nasty C, Suspect 95, Soraia Ramos, Cinema na wengine. Marudio ya hafla hizo yataonyesha kwenye vituo vya BETAfrica, BET international na vituo vya MTV. [3]

Tuzo hizo zimerudisha kipengele cha chaguo la watu. Hafla hizo zilipangwa kufanyika Uganda Februari 4, 2021. Waandaaji wa hafla hizo walitangaza kughairishwa utoaji wa tuzo hizo kupitia ujumbe uliosema "MTV inahofia changamoto za kiafya na usalama"[4]. Hii ni baada ya matukio ya kisiasa yaliuokua yaliendelea nchini Uganda ikiwemo kukamatwa kwa mgombea wa ubunge Bobi Wine[5], iliyopelekea kuanzisha kwa kampeni za kuzuia utoaji wa tuzo hizo. [6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.billboard.com/music/awards/dj-khaled-host-mtv-africa-music-awards-mama-9514671/
  2. https://www.billboard.com/music/awards/dj-khaled-host-mtv-africa-music-awards-mama-9514671/
  3. https://furtherafrica.com/2020/11/28/mtv-africa-music-awards-return/
  4. https://punchng.com/mama-2021-mtv-base-postpones-award/
  5. https://finance.yahoo.com/news/mtv-africa-music-awards-latest-120304686.html
  6. http://saharareporters.com/2021/02/04/bobi-wine-mtv-africa-cancels-music-awards-hold-uganda-petition-reaches-960-signatories
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tuzo za muziki MTV Africa 2021 kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.