Wizkid

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wizkid
Wizkid akitumbuiza katika tamasha la uzinduzi wa albamu ya Iyanya - Desire mnamo 2013
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaAyodeji Ibrahim Balogun
Amezaliwa16 Julai 1990 (1990-07-16) (umri 33)[1]
Surulere, Lagos, Lagos State, Nigeria
Kazi yake
 • Msanii wa rekodi
 • Mtunzi wa nyimbo
 • Mtumbuizaji
Miaka ya kazi2001–hadi sasa[2]
StudioYa sasa

Ya zamani

Ameshirikiana na

Ayodeji Ibrahim Balogun (amezaliwa 16 Julai, 1990), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Wizkid (wakati mwingine hupambizwa kama WizKid),[4] ni msanii wa rekodi, mtunzi wa nyimbo na mtumbuizaji kutoka nchini Nigeria. Alianza kazi ya muziki akiwa na umri wa miaka 11, na kutoa albamu ya ushirika akiwa na Glorious Five iliyopewa jina la Lil Prinz (2001). Mwaka wa 2009, ameingia mkataba na Banky W. iliyo chini ya Empire Mates Entertainment. Ameanza kupata umaarufu zaidi mnamo mwaka wa 2010 baada ya kutoa kibao cha "Holla at Your Boy" kutoka katika albamu yake ya kwanza iliyoitwa Superstar (2011). "Tease Me/Bad Guys", "Don't Dull", Gidi Girl, "Love My Baby", "Pakurumo" na "Oluwa Lo Ni" zilikuwa single kutoka katika albamu ya Superstar. Albamu yake ya pili iliyoitwa , Ayo (2014), ilitanguliwa na vibao kama vile "Jaiye Jaiye", "On Top Your Matter", "One Question", "Joy", "Bombay" na "Show You The Money". Kwa zaidi, katika kazi za kujitegemea, Wizkid amepata kushirikiana na baadhi ya wasanii ambao wamo katika kazi kama vile "Girl" (Bracket), "Fine Lady" (Lynxxx), "Sexy Mama" (Iyanya), "Slow Down" (R2Bees), "The Matter" (Maleek Berry), "Pull Over" (Kcee) na"Bad Girl" (Jesse Jagz).

Kazi na mchango wake katika Tasnia ya Muziki wa Nigeria umepelekea kupata mafanikio kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na tuzo ya BET Award, a MOBO Award, The Headies Awards tatu, Channel O Music Video Awards mbili, nne za Nigeria Entertainment Awards, Ghana Music Award, mbili za Dynamix All Youth Awards, mbili za City People Entertainment Awards, na Future Award. Kwa zaidi, amepata kuchaguliwa mara tatu katika MTV Europe Music Awards vilevile mara nne katika tuzo za World Music Awards. Alipata kuwa nafasi ya 5 kwa msanii mwenye pesa sana wa Afrika mwaka 2013 na jarida la Forbes na Channel O.[5][6] Mnamo Februari 2014, Wizkid amekuwa mwanamuziki wa kwanza wa Kinigeria kuvuka idadi ya milioni 1 ya watu wanaomfuta katika mtandao wa Twitter.[7][8]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Wizkid pops N300m champagne at 23rd birthday bash?. Punch Nigeria. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-10-29. Iliwekwa mnamo 9 October 2013.
 2. Wizkid Biography. MTV Base. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-11-13. Iliwekwa mnamo 12 November 2013.
 3. Nissim, Mayer (11 June 2012). Wizkid: 'Akon is like an older brother to me'. Digital Spy. Iliwekwa mnamo 7 March 2014.
 4. 4.0 4.1 Artists – WizKid. Disturbing London. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-12-13. Iliwekwa mnamo 12 December 2013.
 5. Wizkid richer than 2Face, Banky W – Forbes. The City Reporters (2 September 2013). Iliwekwa mnamo 15 December 2013.
 6. Sarkodie Makes Forbes Top 10 Richest Africa Artistes. The Chronicle (3 September 2013). Iliwekwa mnamo 15 December 2013.
 7. Wizkid- First Nigerian Artiste To Hit A Million Twitter Followers. Modern Ghana (20 February 2014). Iliwekwa mnamo 5 March 2014.
 8. Guess Which Nigerian Artiste Becomes The First To Gain 1 Million Followers on Twitter. Naij News (20 February 2014). Iliwekwa mnamo 5 March 2014.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Kigezo:Empire Mates Entertainment Kigezo:Konvict Muzik