Turf Moor

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa mpira wa Turf Moor

Turf Moor ni uwanja wa mpira wa miguu uliopo Burnley, Lancashire, Uingereza. Ni uwanja wa klabu ya Burnley F.C., ambayo imechezea uwanja huo tangu kuhama kutoka uwanja wao wa zamani wa Calder vale mwaka 1883. Hii inaufanya uwanja wa Turf Moor kuwa Uwanja uliotumika sana kati ya viwanja vya timu 49 zilizowahi kucheza ligi kuu. Uwanja ambao unapatikana katika njia ya Harry Potts, uwanja una uwezo wa kuingiza watazamaji 21,944,wote wamekaa. Ulikuwa kati ya viwanja vya Uingereza kuwa na sehemu ya wachezaji kuingilia na vyumba vya kubadilishia nguo nyuma ya goli moja,mpaka walipoziba kwa ajili ya watazamaji kukaa kwa muda msimu wa 2014–2015 na ulijengwa tena kati ya Njia ya David Fishwick na Njia ya James Hargeaves.

Baada ya vita kuu ya pili ya dunia, uwanja ulikarabatiwa na njia zote nne kujengwa upya.Kwa sasa hizo njia nne ni James Hargeaves, Jimmy McIlroy, Bob Lord na Uwanja wa kriketi.

Burnley F.C. ilicheza mchezo wake wa kwanza kwenye uwanja huo tarehe {17 februari 1883},ilipofungwa 3–6 kwa Rawtensall.Albert Victor alipofungua hospitali Burnley mwaka 1886, Turf Moor ulikuwa uwanja wa kwanza wa mpira wa miguu kutembelewa na Mwanafamilia wa Mfalme wa Uingereza. Mechi ya kwanza ya ligi la Uingereza ilichezwa 6 Oktoba 1888,ambapo Fred Poland alifunga katika Kombe la F.A. mechi kati ya Burnley F.C. na Huddersfield Town. Mwaka huo, Turf Moor ilisimamia nusu fainali ya Kombe la F.A..Mwaka 1927,uwanja ulichezewa katika mechi ya kimataifa kati ya Uingereza na Welisi.

Mwaka 2007,mipango ya kuupanua uwanja uliachiwa katika jamii.Viongozi wa Burnley F.C. walikubariana kuuboresha uwanja kwa Paundi Milioni 20.Mwaka 2009,Burnley F.C. ilichukuliwa kwenda ligi kuu,Paul Fletcher alisema uwezo wa Turf Moor utakuwa 2,800 kutosha watazamaji wa ziada,Lakini timu ilishushwa kutoka ligi kuu mwaka 2010,mipango hii ilisimamishwa.

Baada ya kurudishwa tena kwenye ligi kuu mwaka 2014 uwanja ulianza kukarabatiwa.Tarehe {26 juni 2014} klabu iliachia mipango yake ya kuupanua uwanja sehemu ya kuingilia na kujenga jumba la makumbusho ya timu.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Turf Moor kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.