Tommy Tedesco

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Thomas J. Tedesco (3 Julai, 1930 - 10 Novemba, 1997) alikuwa mwanamuziki maarufu wa Marekani na anayejulikana katika aina yamuziki ya jazz na gitaa.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Gitaa ya aina yenye Tedesco alicheza
Ukulele:mojawapo za ala za muziki ambazo Tedesco aliweza kucheza.

Nyimbo zilizoimbwa na Tommy, tukitaja chache tu, ni myimbo za vipindi vya runinga kama Bonanza, Twilight Zone, Green Acres, M*A*S*H, Batman na kipindi cha Elvis Presley '68 Comeback Special. Alionyeshwa katika vipindi kadhaa vya kuchekesha na ,pia, vya mchezo wa kushindana. Aliigiza kama mchezaji gitaa Tommy Marinucci,mwanachama wa Happy Kyne's Mirth-Makers katika kipindi cha majadiliano cha Fernwood Tonight.

Aliyezaliwa Niagara Falls, New York, Tedesco alisafiri hadi Pwani Magharibi ya Marekani ambapo akawa mmoja wa wachezaji gitaa wa studio wanaotafutwa sana kwa umahiri wake katika miaka ya 1960s hadi miaka ya 1980s. Ingawa kimsingi Tedesco alikuwa mchezaji gitaa, alikuwa anaweza kucheza pia mandolini, ukulele na, vilevile, sitar. Zaidi ya hayo alicheza ala nyingine 28 za kamba.

Tedesco alielezewa na gazeti la Guitar Player kama mchezaji gitaa aliyerekodiwa katika nyingi kabisa katika historia, Tedesco alikuwa amerekodiwa katika maelfu na maelfu ya nyimbo. Alirekodi na wanamuziki bora waliokuwa katika eneo la Los Angeles kama The Beach Boys, The Mamas & Papas, the Everly Brothers, The Association, Barbra Streisand, Elvis Presley, Ella Fitzgerald, Frank Zappa, Sam Cooke, Cher na Nancy & Frank Sinatra. Kwa gazeti laGuitar Player, Tedesco aliandika makala yaliyoitwa Studio Log.Katika makala hayo, alieleza kazina shughuli alizofanya siku hiyo kama kurekodi kipindi cha televisheni, filamu ama albamu huku akieleza vikwazo walivyokumbana navyo, ala za muziki alizotumia na hela kiasi gani alipata kutoka kazi hiyo.

Tedesco alitunga nyimbo za filamu pia kama vile:

  • The French Connection
  • The Godfather
  • Jaws
  • The Deer Hunter
  • Field of Dreams na
  • filamu kadhaa za Elvis Presley.

Yeye, pia,alikuwa mchezaji gitaa wa Original Roxy katika kipindi cha The Rocky Horror Show. Zaidi ya hayo, yeye alicheza gitaa katika mwanzo wa filamu ya Howard Hawkes & John Wayne iliyoitwa Rio Lobo. Alikuwa mmoja wa watu waliofanya kazi ya kando waliopewa sifa na heshima katika kazi yake katika katuni ya The Ant and the Aardvark(1968-1971).

Akiwa pekee yake,Tedesco alirekodi albamu kadhaa katika mtindo wa kucheza jazz gitaa lakini kazi yake ya kimuziki iliisha alipopata shtuko la moyo liliomfanya kufa ganzi katika sehemu kadhaa za mwili yake. Mwaka uliofuata alichapisha tawasifu yake yenye jina la Confessions of a Guitar Player.

Tommy Tedesco alikufa katika eneo la Northridge, California katika mwaka wa 1997, akiwa mwenye umri wa miaka 67, kutokana na saratani ya mapafu.

Tedesco, pamoja na wanamuziki wenzake wengi wa studio,walihusika katika filamu ya dakika 95 ya 2008 The Wrecking Crew iliyoundwa na mwana wake, Danny Tedesco. Filamu hii imeonyeshwa katika matamasha kadhaa lakini bado haijatolewa kibiashara.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]