Theofilo Kijana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Theofilo Kijana (alifariki 30 Januari 792) alikuwa askari aliyewekwa kusimamia kituo cha kijeshi cha kisiwa cha Kupro[1].

Baada ya kukamatwa na Waarabu, alikataa kusilimu kwa zawadi na kwa vitisho akafungwa gerezani miaka 4. Hatimaye aliuawa kwa upanga[2][3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 30 Januari[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.