Nenda kwa yaliyomo

Themistokle wa Myra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Themistokle wa Myra (alifariki Myra, leo nchini Uturuki, 251 hivi) alikuwa mchungaji wa mji huo aliyeuawa kwa ajili ya imani yake ya Kikristo katika dhuluma ya kaisari Decius[1].

Inasemekana kwamba alijitambulisha kuwa Mkristo ili kumlinda Dioskoro, aliyetafutwa ili kuuawa, na kwamba, kisha kuteswa kikatili, kuburutwa barabarani na kupigwa mijeledi, aliuawa[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Tarehe 21 Desemba ndiyo sikukuu yake[3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.