Taiwan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Taiwani)
Ramani ya Taiwan

Taiwan (pia: Taiwani, Formosa) ni kisiwa cha Asia ya Mashariki katika Pasifiki. Iko upande wa kusini-mashariki wa China, kusini kwa Japani na magharibi kwa Ufilipino.

Jina la zamani la Taiwan lilikuwa "Formosa" (kwa Kireno: kisiwa kizuri, cha kupendeza).

Taiwan ni pia sehemu kubwa ya eneo la Jamhuri ya China iliyoenea kwenye visiwa vingine vidogo nje ya China bara.

Miji mikubwa ni Taipei na Kaohsiung.

Wakazi walio wengi ni Wachina wa Han. Kuna pia wakazi asilia waongeao lugha tofautitofauti.

Kisiwa kinadaiwa na Jamhuri ya Watu wa China kama eneo lake.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Taiwan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.