Tombo
Mandhari
(Elekezwa kutoka Synoicus)
Tombo | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 4, spishi 16:
|
Tombo (pia tomboo au tomboro) ni ndege wadogo wa jenasi kadhaa katika familia ya Phasianidae. Rangi yao ni kahawia na wana michirizi. Spishi nyingine zina rangi nyekundu na buluu. Kabla ya kuruka angani hungoja mpaka mtu ni karibu kuwakanyaga na huenda umbali fupi tu. Hula mbegu hasa lakini pengine hukamata wadudu pia. Hutaga mayai 6-18 ardhini.
Tombo wanatokea Afrika, Australasia na Ulaya. Kuna ndege huko Amerika ambao wana mnasaba na tombo, lakini wanaainishwa ndani ya familia Odontophoridae.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Coturnix coturnix, Tombo wa Ulaya (Common Quail)
- Coturnix c. africana, Tombo wa Afrika (African Quail)
- Coturnix c. coturnix, Tombo wa Ulaya (Eurasian Quail)
- Coturnix c. erlangeri, Tombo Habeshi (Abyssinian Quail)
- Coturnix c. inopinata, Tombo wa Kaboverde (Cape Verde Quail)
- Coturnix delegorguei, Tombo Kidari-cheusi (Harlequin Quail)
- Perdicula asiatica, Tombo wa Asia (Jungle Bush-quail) imewasilishwa katika Reunion
- Synoicus adansonii, Tombo Buluu (Blue Quail)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Coturnix coromandelica (Rain Quail)
- Coturnix japonica (Japanese Quail)
- Coturnix novaezelandiae (New Zealand Quail) imekwisha sasa
- Coturnix pectoralis (Stubble Quail)
- Ophrysia superciliosa (Himalayan Quail) labda imekwisha sasa
- Perdicula argoondah (Rock Bush Quail)
- Perdicula asiatica (Jungle Bush Quail)
- Perdicula erythrorhyncha (Painted Bush Quail)
- Perdicula manipurensis (Manipur Bush Quail)
- Synoicus chinensis (King Quail)
- Synoicus monorthonyx (Snow Mountain Quail)
- Synoicus ypsilophorus (Brown Quail)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Tombo wa Ulaya
-
Tombo kidari-cheusi
-
Tombo wa Asia
-
Rain quail
-
Japanese quails
-
Stubble quail
-
Rock bush quail
-
Painted bush quail
-
King quail
-
Snow mountain quail
-
Brown quail