Tandu-shamba
Mandhari
(Elekezwa kutoka Symphyla)
Tandu-shamba | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Spishi isiyotambuliwa ya Symphyla
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Familia: |
Tandu-shamba ni aina za arithropodi wadogo katika ngeli Symphyla ya nusufaila Myriapoda. Hata kama wanafanana na tandu wa kawaida, inaonekana kwamba wana mnasaba zaidi na majongoo lakini uchanganuzi wa ADN umetoa matokeo yanayopingana. Hawa ni wanyama wadogo wenye mm 2-30. Mwili wao ni mwororo na unapenyeka kwa nuru. Hawana macho na hutumia vipapasio ili kusikia njia. Huonekana katika udongo mpaka kina cha sm 50. Hula dutu ya viumbehai lakini spishi kadhaa zinaweza kuharibu mimea ya shambani.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Scutigerella immaculata