Swaziland Kids Rugby Mission
Swaziland Kids Rugby Mission (SKRUM) ni shirika lililoanzishwa na Michael Collinson kutoka Yorkshire mnamo mwaka 2008 kama shirika lisilolenga kupata faida ambalo hutumia mchezo wa raga kuwashirikisha watoto na kuwafundisha juu ya muamko wa kijinsia na elimu ili kuzuia kuenea kwa VVU.[1]
Michael Collinson, mchezaji wa zamani wa raga na mkufunzi/kocha alipooza katika ajali ya gari mnamo mwaka 2002. Baada ya kupigana kwa miaka kadhaa na unyogovu, alitambua ni kiasi gani VVU / UKIMWI vilikuwa vinaathiri watu wa eneo hilo akaanzisha SKRUM kutumia raga kama nyenzo ya kufundishia dhidi ya VVU / UKIMWI.[2]
Tangu kuanzishwa kwake, SKRUM imetembelea shule 650 kati ya 817 nchini Eswatini na kuwafikia vijana 12,000 kila mwaka kupitia juhudi za ufikiaji wa shule na jamii.[2] Kauli mbiu ya SKRUM ni "Pitisha Mpira Sio Virusi."[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Fundraiser for Swaziland rugby project launched at Crumlin school". South Wales Argus (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-08.
- ↑ 2.0 2.1 Aimee Lewis CNN. "How rugby is helping tackle HIV Aids in Swaziland". CNN. Iliwekwa mnamo 2021-08-08.
{{cite web}}
:|author=
has generic name (help) - ↑ "Appeal brings joy of sport to young in Africa". Okehampton Times (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-08-08. Iliwekwa mnamo 2021-08-08.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |